BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, December 6, 2010

AMPLIFIER SHOW MPYA KUTOKA KWA MILLARD AYO CLOUDS FM.


LEO katika pita pita zangu katika kusikiliza Radio za hapa kwetu TZ nimepata nafasi ku tune katika 88.4 Clouds Fm peoples station mida ya saa moja hivi na nimepata kusikia sauti ya mtangazaji ambaye nilikuwa nimemiss kwa muda sauti yake, anafahamika kama MILLARD AYO  aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Radio cha Radio 1 stereo hivi sasa ni mwajiriwa  mtangazaji wa kituo cha  radio cha Clouds fm na leo alikuwa katika show yake mpya ya AMPLIFIER ambayo imeshika nafasi ya kipindi cha BAMBATAA kilichokuwa kikiongozzwa na mwanadada Sofia Kessy hivi sasa hakitakuwepo tena na badala yake wapenzi wa station hii tutapata nafasi ya kusilia kipindi hiki cha Millard kila siku za wiki kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku j3 hadi ijumaa.



Kijana huyu amekuja kivingine kabisa na show yake ni bonge la show zaidi ya ile aliyokuwa nayo Radio nayo ya Milzo 101.Pia kuanzia January 2011 atakuwa na show yake mpya kupitia kitua cha televisinon cha Clouds TV.

0 comments: