BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, June 19, 2010

NGOSHA ZE SWAGGA DON LYRINCS

Ngosha ze swagga Don LYRICS

ntro
Fid Q: So Swagtastik!!!
Naj: Ngosha ze Swagga Don x4
Verse 1:
(Fid Q)
Mc’z wanaenda down, ka Zim(babwe) dollars/
Mie sio bling, mie culture ka ZEMKALA/
Da brightest thang shining next to a diaMOND/
Niite Ghost Writter ninapo Blaze ka AMO/
Mara nyingi mie nina bahati kama Lotto Machines/
Si mtu wa adventures kama Frodo kwenye Lord of the Rings/
Niite Roscoe, ninapoSPEAK in Tongues ka Jenkinz/
Don kama Bosco, Mad kama Ice Helsink/
Unataka Bed fight? Mie nina King size na French fries kwa Breakfast/ T- bone stake na PRISON BREAK kiGangstar/
Tattoo plan kama Michael Scolfield/
Bruce lee wa Rap ya Africa, Rock city naigeuza Rap City/
Nina Gucci Lips namaanisha ziko Brown/
Materialistic wanapenda niwe around/
Sexy & Single na pia hufurahi nikiwa FREE/
Nilipenda 3 sum zaidi ya unavyoipenda track hii/
Trust me, ninahitaji wife and some gorgeous Kids/
Seen, mie sio bogus we una dance ka Lotus juu ya hii beat/
Mashairi kwangu Pipi, nayagawa ka Santa Claus/
Kazi na Dawa Marco puff 3 kitu BOUNCE/
Mademu hawapendi kuona unavyomdiss FID/
Wote nawaita Candy sababu they’re so SWEET/
I’m so 2010 sihitaji Pad or Pen,u so 2000 and late/
Na haulipuki ka Bin Laden/

Chorus:
( Naj) Ngosha ze Swagga don x8
2nd Verse:
(Fid Q) My Mama.. didn’t raise no Fool/
Ninavyo Bust a Rhyme… wananiita Leader wa new School/
Ngosha ze SWAGGA DON.. Uh uh usinidownload/
Hapa utapata ladha expensive zaidi ya iPhone/
Mie sio Superstar ni International I con/
I’m Internationaly known kama Tyson/
Flow iko so Universal kama yvone, CHAKA CHAKA/
Ladies and Gentlemen ni Rappers Rapper hapa/
Naweza kwenda Quick kama ROCKA nikawatisha kisha mkaa ‘’ We Love you FIDQ’’ U deserve girls… Q yuko stronger ka playa wa Baseball au Wrestling/ usiniite Paper Chaser mie nina Chase Dreams/
Kama una Pesa Jenga kabla haujaanza Pimp Rimz/
Jikomboe kama wanaojiunga na X treme/
Drive with care, coz Life has no Spare/ na piiiiiiiiaaaaaaa…,.
‘’ THEY SAY IM COOL LIKE FIRE & AND IM HOT LIKE ICE OH UYEAH… U FEEL WHAT I SPEAK COZ I SPEAK WHAT I FEEL OH YEAH’ X2

HISTORIA YA BONGO FLEVA SEHEM YA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA

Moja kati ya mambo niyapendayo mno maishani ni muziki.Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa muziki si tu ule wa nje lakini kwa karibu ule wa nyumbani hasa muziki wa dansi na ule wenye umaarufu sana hivi sasa ujulikanao kama Bongo Flava (Muziki wa Kizazi Kipya).Katika mapenzi hayo imekuwa kama bahati kuwa mmoja wa vijana wengi tuliobahatika kuuona muziki huu wa kizazi kipya ukizaliwa na pengine bahati zaidi bila kusita kusema;kuwa mmoja kati ya wale tulioanzisha kusukuma gurudumu la muziki huu kufikia hapa ulipo na nafasi yake kutambulika si tu Afrika Mashariki bali pia kwa sasa duniani kwa ujumla.
Kama ilivyo kwa aina zingine za muziki Tanzania,mfano muziki wa dansi basi utakuwa mkosefu wa fadhila bila kujumuisha majina kama Patrick Balisidya,Mbaraka Mwaruka Mwinshehe,Salum Abdalah na hata Remmy Ongara.Hawa ni vinara na walifanya kila wawezalo kuja na ubunifu si tu kuvutia wateja wao bali kuutangaza muziki wao ndani na nje ya nchi na kuipa Tanzania kitambulisho chake kwenye jukwaa la sanaa ya muziki.Kazi za wanamuziki hawa zilifana sana kwa ushirikiano mkubwa na chombo ambacho kwa Tanzania ni muhimu sana katika kueneza au kutambulisha kitu kipya,RADIO.Watangazaji kama Mzee Ibrahim Chimgege,Enock Ngombale,Timothy Pata,Abisai Stephen,Seif Salum Nkamba na Julius Nyaisangah chini ya ma-bwana mitambo mahiri kama akina James Mhilu na Crispin Lugongo wanastahili pongezi kwa kiasi kikubwa katika kurekodi na kusimamia mitambo wakati wanamuziki hawa wakitafuta majina na namna ya kujitambulisha kwa jamii itakayosikiliza muziki wao.Bahati mbaya huwasikii sana watu hawa katika zinazoitwa historia kwa sababu wengi ni rahisi kuwasahau lakini mchango wao ni mkubwa sana na unastahili heshima hasa unapoandika au kuizungumzia historia ya muziki wa dansi Tanzania.
Nimetoa mfano wa hali halisi kwa ufupi kuhusu muziki wa dansi ili kukupa nafasi ya kujua kwa undani kile ambacho kinakweza kichwa cha habari hapo juu.Nia yangu hasa ni kuandika yale niliyoyaona na uzoefu wangu katika muziki huu wa sasa maarufu kama Bongo Flava.Muziki huu umeshika kasi na unapendwa sana hivi sasa kila kona.Ni faraja kuona hata wale walio ughaibuni siku hizi si ajabu kumkuta mtu ana albamu jpya la mwanamuziki wa Bongo Flava akiicheza ndani ya nyumba yake au garini kwa fahari.Inafurahisha kuona mapenzi kwa muziki huu yamekuwa makubwa na hilo ndilo lengo kuu.
Pamoja na yote haya,kama ilivyo kwa kila jambo ni vyema historia yake ikawa nyoofu na si kama ilivyo sasa ambavyo imekuwa ikipindishwa pindishwa mno,sijui kama ni kwa makusudi au kwa wengi kutojua harakati na wanaharakati walioufikisha muziki huu hapa ulipo.Kwa kuandika kwa usahihi yale yaliojiri juu ya chimbuko la muziki huu tutakuwa tunawatunzia wanetu na wengineo haki ya kuuelewa na kuutukuza zaidi muziki huu na msimamo wake katika jamii ya leo na ijayo.Shukrani labda nizitoe kwa Kaka Bonny Makene na Uncle michuzi kwa kunisukuma kujaribu kuandika nikijuacho juu ya muziki huu.
Kama nilivyododosa hapo juu kuhusu muziki wa dansi basi sasa niingie kwenye muziki huu wa kizazi kipya.Muziki huu ni ule ambao unajumuisha mitindo mbali mbali ambayo zamani tulizoea kuona ikipigwa na watu wa nje ya Tanzania kuanzia Hip Hop,R&B,Zouk na hata Soul.
Katika Hip Hop ya Tanzania pia utakosa fadhila kama hutotaja vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mivao yao na kufoka foka kwao kulikuwa ni burudani na ushawishi tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu maana halisi ya utamaduni huu hasa Tanzania.Kwa wakati huo ilionekana kama uhuni tena wa kupita kiasi.Nitawataja wachache ninaowakumbuka ambao kila kukicha ukigongana nao kwenye Night Clubs,Samora Avenue pale Salamander basi ulikuwa unachoka mwenyewe.Nakumbuka vijana kama John Simple,Dj Rusual,The BIG One,Babu Manju,David Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom London,OPP (now Jay P) na Dj Ngomeley.
Tukiendelea hao niliowataja hapo juu walikuwa chachu katika uvaaji wa kihip-hop na katika kughani na sijui kama kuna mtu atasahau watu kama Fresh XE Mtui,BBG (alianza na Mr II),Adili kumbuka,KBC (Mbeya Tech),Saleh Jabir,Samia X,THE BIG,Rhymson,2Proud.Deplowmatz na wengineo wengi ambao walikuwepo na wakighani katka school parties au matamasha ya mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio.
Kwa mara ya kwanza pia promoters kama Joe Kusaga na Abdul hakim Magomelo walionekana kutobaki nyuma katika ukuzaji wa sanaa hii ambapo waliandaa matamasha mbali kama Yo! Rap Bonanza na Coco beach Bottle Parties kwa ajili ya kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa kughani.Matokeo yake yalikuwa ya kufurahisha kwani kila mmoja alikuwa na shauku ya kuingia katika gemu.
Kwa vile sio watu wote walikuwa na uwezo wa kughani lakini pia kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali kwenye Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yalikuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.Hapa tunakumbuka kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wake wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimpa tafu hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye instrumental (ala) tupu aliyonipatia kama zawadi aliporudi toka UK kwani instrumental ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba.
Naweza nikawa nimesahahu majina machache hapo juu lakini kwa ufupi hao ni baadhi ya watu wa mwanzo kabisa kuuingiza masikioni mwa jamii muziki wa kizazi kipya pengine hata kabla ya chombo kilichoipaisha juu zaidi..RADIO.Na ninaposema Radio simaanishi Radio nyingine bali Radio One Stereo kama Radio pekee yenye kujivunia juu ya ukuaji wa muziki huu wa kizazi kipya kufikia hapa ulipo.
Lakini uko nako hakukuwa na mteremko,mambo yalikuwa mengi na mazito mpaka muziki kujipenyeza na kukubalika.Je nini kilichochea mapambano ya kuuchomeka muziki huu Radioni na kuupa nafasi ya kupigwa sambamba aina zingine za muziki kama ule wa dansi nk? nani alihusika katika harakati hizo na nini kilifuata? ugumu huo ulitokana na nini?

HISTORIA YA BONGO FLEVA SEHEM YA MWISHO
SEHEMU YA MWISHO
Kufikia hatua hii basi labda niseme tu kuwa imefika wakati wanamuziki wa Hip Hop na Bongo Flava leo hii wana nafasi yao katika jamii ya Tanzania na wanapaswa kuenziwa,kukumbukwa na kuheshimika bila kuchanganya aina hizi mbili za muziki kwani ni vitu viwili tofauti kabisa lakini lengo likiwa moja.Kuna mambo mawili ambayo nadhani yakifanyika basi angalau kumbukumbu ya wale wakongwe walioanzisha harakati na mapinduzi katika muziki huu watadumishwa na wale wapya watajifunza kutokana na kuwaenzi wakongwe hawa.
Hapa tusisahau pia wakongwe waliokuwa wakipiga ianyoitwa Hard Core HipHop kama Fresh XE ambaye sidhani kama alibahatika kurekodi,Samia X,GWM,E-Attack,Underground Soul,Hasheem,KU Crew,Nigga One,D-Rob au II Proud na wengineo ambao walikuwapo hata kabla ya kipindi cha DJ SHOW au Radio One kuanza lakini hawakuwa na sehemu ya kuutangaza muziki wao.Hawa kamwe hawatasahaulika na wana heshima kubwa sana kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.
Bila kutegemea “Awards” ambazo zinaonekana kuwa na dosari kila zinapofanyika kila mwaka kwa tuhuma za upendeleo nadhani imefika wakati mwafaka kwa muziki huu na wanamuziki wake kuwa na tuzo zake maalum zitakazofanyika kila mwaka na kuzitofautisha kabisa na zile tulizozioea za muziki mchanganyiko.
Kuwepo na utaratibu wa kujumuisha wiki ya tuzo hizo na usaidiaji wa jamii kwa wakongwe watakotumikiwa tuzo hizo kutembelea baadhi ya shule za msingi au sekondari na kutoa changamoto ya maisha na elimu juu ya muziki huu kwa ujumla kwa kizazi hiki kijacho.Pia hata kushiriki nao katika shughuli za usafi wa mazingira kwa siku hiyo.Huu ni mchango tosha na ishara kuwa muziki huu si uhuni ni sehemu ya maisha kwa kizazi kipya.
Vile vile sehemu ya mapato na udhamini wa onesho hili iende kusaidia shule masikini au ya watoto wasiobahatika na wenye ulemavu wa namna moja au nyingine.
Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu

USIJE MJINI LYRINCS/MWANA FA&AY

USIJE MJINI LYRICS / MWANA FA & AY

Verse I…
Ogopa matapeli nyumba hii haiuzwi/
Moja ya nembo maarufu hapa mjini mzazi/
Wote tunataka utajiri so zinatungwa mitkas/
Watu wanalia kila siku ka matarumbeta ya arusi/
Jua limeshushwa zaidi mjini/
Na huwaka zaidi mifukoni/
Kila Malaya ana story na zote huwa hazifanani/
kumbuka Zubeda/Yule binti wa Professor/
akashindwa jua atamsaidiaje mjini kuna mengi brother/
wanachapa mpaka ndala/kwenye nyumba za ibada/
sio wote wana pa kulala usidanganywe na luninga/
huku huku kwenye ufisadi waliopo hawataki kurudi/
hata mbunge wa kwenu yupo huko atakuja uchaguzi/
sio wote mambo ni safi wengine wamegomewa na maisha/
wanaona haya watarudije na story walizowahisha/
hakuna shamba hakuna mbuga labda kuwaibia wajinga/
mawazo yatayofanikiwa ni moja ya kumi ya unayoyafuga/
so they say…..

Choras..
yafaa uskize nnayosema/huku kugumu unaweza kupotea/
nananananana (usije mjini)
nananananana (nishakwambia usije mjini)
eeeeeh eeeh (usije mjini)
eeeeeh eeeh (nishasema usije mjini)
eeeeeh eeeh (usije mjini)
eeeeeh eeeh (narudia tena usije mjini)


VERSE II
Maisha ya huku ni mbinde
Yafaa kutumia akili ya kuzaliwa ndio ushinde
Watu wanahustle everyday
Wapunguze makali ya maisha day after day
Kuna wivu,chuki,ghasia,fitina
Watu wako mbio mbio kupoteza muda hakuna
Wanatoroka na wake hata waume wa wenzao
Wengine hawatosheki wanawachapa mpaka watoto zao
Mbwebwe nyingi vyeti feki wengine wakikopa hawalipi
Na si wote wanaosmile ukadhani wako happy
Hawamaanishi ila ubishi
Maisha hayana hata urafiki
Bora bush town uzushi huko undugu huku cash
Town nani hana deni
Kama hauna kazi muda nao hauendi
Na si kila aliye town basi mjanja
Unaweza kuukamata mkwanja
kisha ukaonekana mshamba
usije mjini son

Verse III..
Daisaama samba m’magai/kama mbwai mbwa/
Kuni ni watu jua ndio moto sikutishi mji haufai/
Wamasai hawachungi ng’ombe huku wanalinda magari/
Washaiba deal ya wamakonde mji ulivyokuwa nishai/
Siku hizi hawawindi simba wanasuka dada zetu tu/
Mjini huwezi kuwa mtu kama huna deal ya mkwanja mkuu/
Nafuu huko kuna waganga kweli/huku hata dini ni dili/
Na kuna manyoya cuz mjini sio kuzuri/
Na si kila alie town basi mjanja/
Unaweza ukaukamata mkwanja halafu ukaonekana mshamba/