BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Thursday, November 17, 2011

SAFARI YA TIMU YA TAIFA YA POOR YAKAMILIKA...


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kuondoka kwa  timu ya Taifa katika mashindano ya All africa Cup 2011 Blantyre Malawi yanayotarajiwa kuanza tarehe 22.11.2011 mpaka 26.11.2011.


Akitangaza safri hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Bw Oscar Shelukindo alisema kuwa tayari wamekamilisha yale mahitaji yote muhimu ya Timu ya Taifa kwa ajili ya safari hiyo.


Bw Oscar alisema kuwa Safari Lager ndiyo mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imekuwa ikiidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa pool table tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Africa na Dunia. 


“Timu itapita katika mikoa ifuatayo na kucheza mechi za kirafiki na timu za mikoa. Mikoa hiyo ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Kyela- Mbeya na Kasumulo boarder- Mbeya kwahiyo ni muda mwafaka kwa wananchi kuangalia timu yenu na kuona jinsi ilivyojiandaa. 


Naye kocha mkuu wa timu ya taifa, Ndugu Denis Lungu alitangaza majina ya wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kuondoka leo kua ni Omary Akida kutoka Kinondoni, Felix Atanas(Dodoma), Godfrey Mhando (Kinondoni), Mohamed iddy (Kinondoni),Charles venance ambaye ni captain toka Temeke.


Wengine ni Antony Thomas kutoka Ilala, Shamis nasorro (Ilala) pamoja na Abdallah Hussein wa Kinondoni.


Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema kuwa katika mashindano ya mwaka huu ya ALL AFRICA CUP yanatajiwa kushirikisha nchi 14 wanachama wa All Africa Pool Association (AAPA) na nchi hizo ni Africa kusini, Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda, Swazland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria , Msumbiji,  Morocco na  Lesotho.


Akitoa salamu za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho alisema  kuwa mchezo wa pool table sasa umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama michezo mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania.


“ Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuiweka Tanzania katika ramani ya michezo kimataifa kupitia SAFARI LAGER BEER ni fahari kubwa kwa mchezo wa pool table Tanzania. TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”

MLIMBWENDE WA LEO…


Anaitwa Suzan Marala anasomea Shahada ya Social protection katika chuo kikuu cha IFM ana ndoto kibao ikiwemo kuwa meneja katika mifuko ya hifadhi ya jamii.


Anapenda kubadilishana mawazo, kusoma riwaya, kusikiliza na kucheza muziki na pia kuchat na marafiki.



Kama unapenda kuwa mrembo wa siku katika blog hii usisite kunitumia picha kiupitia email ambayo ni famanmawenya@yahoo.fr

Tuesday, November 15, 2011

BREKING NEWZ.. MOTO WATOKEA DAR MAENEO YA MITAMBO YA TANESCO...


Moto mkubwa umetokea leo maeneo ya Tanesco makao makuu na kuteketeza transofrmer moja ambayo ilikuwa inaregurate umeme kwa mkoa wa DSM na Unguja hivyo kwa kmujibu wa Bi sophia Mgonja athari ya moto haijajulikana na chanzo chake na jitihada za kurudisha umeme zinafanyika japokuwa haijajulikana utarudi lini...

Hivyo wakazi wa DSM na sehemu zingine wata xperience adha hiyo kwa muda usio julikana..