BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, August 14, 2011

P SQUARE WAVUNJA REKODI NA ALBUM YAO YA INVASION....


Wasanii twins Peter na Paul Okoye aka P-Square,wamepiga bonge la show wakati wa uzinduzi wa album yao mpya ya 5 pande za Expo Hall - Eko Hotels na kuvunja rekodi ya mauzo kiaina....nchini humo!


Album yao inaitwa Invasion,na ilikua kitaani Jumatano iliyopita na mpaka kufikia Jumamosi walikua wameshauza kama copy milioni 1 hivi...na wadau wa Nigeria wanasema kuwa huenda wakavunja rekodi ya mauzo kwa album zao zote 4 walizowahi kuzitoa tangu walipotoa ya kwanza mwaka 2003 ya Last Nite.

NAMKUBALI HUY DADA KWA KAZI YAKE...

Anaitwa Kijakazi Yunus ni Mtangazaji wa Kipindi cha AFROBEAT kupitia Eatv kila j'mosi saa 1 jioni.

na pia hutangaza kipindi cha AFROSUNDAY ya EARadio Jumapili saa 12 jioni mpaka 3ucku...

TSJ YAANDAA MASHINDANO YA MISS & MR KWA MWAKA HUU....



SERIKALI ya wanafunzi ya Time School of Journalism (TISJOSO) kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya Zealot Entertainment Agency imeandaa mashindano ya urembo ya kumtafuta mshindi na mwakilishi ya kinyang’anyiro cha Miss na Mr TSJ 2011.


Shindano hilo litafanyika katika sherehe ya Welcome First Year Special Bash ambayo imelenga kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo kwa ngazi zote kuanzia Basic Certificate, Advanced Certificate na Diploma kwa mwaka huu.


Hafla hiyo ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza ambayo itapendezeshwa na mashindano haya inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Septemba mwaka huu katika maeneo ya Jangwani Sea Breeze Mbezi beach.

Mshindi wa shindano la Miss Tsj 2010 Lilliana Andrew.



Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na serikali ya wanafunzi kwa ajili ya washiriki na kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Naibu Waziri wa Michezo wa TISJOSO Bi. Frida Matinya alisema mashindano ya mwaka huu ni mashindano rasmi na yako tofauti na mashindano yaliyowahi kufanyika hapo awali.


Bi Matinya alisema kuwa mashindano yaliyokuwa yakifanyika mwanzoni yalikuwa hayana tija kwa washiriki kwani hayakuwawezesha kupiga hatua yoyote ya kuendeleza kipaji hicho licha ya kuwa kuna baadhi ya waliofanikiwa kuendelea katika tasnia hiyo kama Lillian Andrew ambaye aliweza kushirirki katika kinyang’anyiro cha Miss Tabata 2010 na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu.


“Tunatarajia kuyaboresha mashindano haya na mwaka huu kutakuwa na zawadi nzuri sana kwa kuwa tumeweza kuwa na mawasiliano mazuri na baadhi ya kampuni ambazo zinaelekea kudhamini mashindano haya,”alisema Matinya.


Aliongeza kuwa kamati yake pamoja na serikali ya wanafunzi inajaribu kutafuta mahusiano mazuri na waratibu wa mashindano makubwa ili kutoa nafasi kwa TSJ kuwa na warembo wanaowakilisha chuo hasa kwa Miss Tanzania ambayo ni mashindano makubwa yanayoendelea.
Mshindi wa shindano la Miss Tsj 2010 Lilliana Andrew


Mpaka hivi sasa washiriki waliojitokeza ni 11 na tunazidi kuwahimiza wajitokeze kuchukua fomu ili washiriki katika mashindano hayo na wao watambue kuwa mashindano haya humpatia cheti cha heshima mshindi  na cheti hicho ni kama utambulisho ambacho mbali na zawadi pia kitampa nafasi ya kuonyesha ushiriki wake katika mashindano hayo.


Tunatarajia kuwa washiriki hawa wataingia katika mazoezi ya maandalizi ya shindano hili wiki mbili kabla ya tukio na siku tatu kabla ya tukio tutatangaza zawadi za washindi watakao ingia katika fainali hiyo.


Hata hivyo, Waziri wa Habari wa serikali ya wanafunzi TISJOSO Bi Jestina Joseph, alisema mbali na mashindano hayo pia katika sherehe hiyo kutakuwa na mashindano mbali mbali ambayo yatatoa nafasi kubwa kwa wanafunzi kufurahia hasa kuwaweka karibu na wanafunzi ambao wameingia chuoni.


“Lengo la sherehe hii ya Welcome First Year Special Bash kwa mwaka huu ni kuwaweka wanafunzi karibu na pia kujijenga kisaikolojia kwani michezo hujenga na kujumuika pamoja katika hafla hii itatuwezesha kuwa na ushirikiano wa kutosha,” alisema Bi Jestina.


Aliongeza kuwa pia sherehe hii itakuwa sehemu mojawapo ya kusherehekea ushindi uliopatikana katika mashindano ya taaluma ya utangazaji yaliyofanyika hivi karibuni katika chuo cha Royal College of Tanzania (RCT) na chuo cha TSJ kiliibuka mshindi wa mashindano hayo.
Mshindi wa shindano la Miss Tsj 2010 Lilliana Andrew (kulia) akiwa na mshindi wa pili wa shindano hilo Benardina Mwita( katikati) na mmoja wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TSJ (kushoto).


Alieleza kuwa chuo cha TSJ kiliona ni vyema kushiriki katika mashindano haya ili kujenga uelewa wa taaluma hii na kuona jinsi vyuo vingine wanavyofundishwa katika taaluma hii.


Aliongeza kuwa mbali na kuburudika kwa michezo mbali mbali katika sherehe hiyo ni wakati wa kukutana pia na waandishi pamoja na wahariri wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa Tanzania kuzungumza nao ili nao watupatie elimu itakayo waandaaa kuelekea kazini.


“Tunatarajia kualika wadau mbali mbali wa habari ambao tutajumuika nao pamoja katika sherehe hii ili kubadilishana nao mawazo na kujifunza mengi kutoka kwao na pia tutakuwa na mgeni rasmi kutoka serikalini ambaye tutawajulisha baadae ni nani atakaye kuja kwani bado tuko katika mawasiliano nae,” aliongeza.
  Mshindi wa Miss TSJ 2010 Lilian Andrew (kulia) ambaye pia ni mshindi wa tatu katika shindano la Miss Tabata 2010 akiwa na mshindi wa kwanza wa Miss Tabata 2010 Consolata Lukosi (katikati) na mshindi wa pili wa shindano hilo Cynthia Shayo (kushoto).