BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Tuesday, October 12, 2010

Nane waingia fainal, wapata fursa ya kuonyesha kazi zao jukwaa la Swahili Fashion Week 2010.


Contemporary Swahili” ni kauli mbiu ya shindano 2010  
Hatimae majina ya wabunifu 8 wenye vipaji  ambao wameingia fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika  onyesho kubwa la wiki la mavazi  Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.
   
Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 10 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 8 yalichaguliwa na jopo la majaji  wanne  ambao ni Jamila Swai ambae ni mbunifu wa mavazi hapa nchini, Mkurugenzi wa Sanaa Nsao Shalua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council), Michelangelo Adam kutoka ubalozo wa  Italia hapa ncini na Mustafa Hassanali.  
  
Wabunifu hao 8 waliongia fainali watashindana  katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
  
Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “  Wabunifu wote 16 walikuwa wazuri  na wameonyesha vipaji vya hali ya juu, na  kuonyesha kuaTanzania ina vipaji vikubwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi”.

Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali ni pamoja na Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urassa, Shaban Mfaume, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Angelina Muna and Grace Kijo.

Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza  kupitisha majina 8 ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika  kuangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.

Swahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi  na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba  na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .

Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.