BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Wednesday, December 21, 2011

MAAFA DAR..







Sunday, December 18, 2011

BADEF WAZINDUA KAMPENI YA UELEWA JUU ALBINO..


Mbunge   wa Lindi Mjini Salum Barwany akizungumza wakati mkutano na waandishi jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya chakula kwa ajili ya harambee ya  cha kuchangia Sh500millioni kwenye mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu wa ngozi  wa Barwany Albinism  development trust fund (BADEF), hafla inatajiwa kufanyika mwenzi wa pili mwaka ujao. Kushoto ni Mtunza fedha wa BADEF, Thomas Monji na kulia nimsaidizi wa Mbunge, Godfrey Mbowe. 

Tuesday, December 6, 2011

AJALI MBAYA YATOKEA MANDELA ROAD MAENEO YA RELINI MWANANCHI...

Abiria waliojeruhiwa wakipelekwa hospitali baada ya kupata ajari kwenye daladala aina ya Hiace yenye namba za usajiri T 214 AST linalofanya safari kati ya T/Hai na M/Sita,ambapo liliacha barabara na kugonba kituo eneo la Tabata Relini na kusababisha kifo cha mtu mmoja papo hapo jijini Dar es Salaam jana.
Wasamalia wema wakijaribu kuwanasua abiria waliokuwa kwenye daladala aina ya Hiace yenye namba za usajiri T 214 AST linalofanya safari kati ya T/Hai na M/Sita,ambapo liliacha barabara na kugonba kituo eneo la Tabata Relini na kusababisha kifo cha mtu mmoja papo hapo jijini Dar es Salaam jana.


Mwili wa marehemu aliyefariki kwa ajali ya gari ambaye jina lake halikufahamika haraka

MAI AFUNGUKA...


MWANADADA anayetesa katika Komedi Bongo, Mai Ali Mai Dread, amelazimika kuikimbia kambi ya kundi lake la Vituko Show iliyopo jijini Mbeya akidai imejaa majungu.

Msanii kwa sasa anafanya kazi na Bongo Super Stars Comedy.
Nimekimbia kambi kwa sababu ya majungu, si unajua wanawake tukiwa pamoja? Lazima majungu yawepo. Ni balaa fulani hivi limeingia, alisema Mai Dread.

Awali nilipokuwa na akina Asha Boko, Bi. Rehema na wengineo, tulifanya kazi vizuri tu, lakini walivyoingia wasichana tu, mambo ya wivu yakaanza.

Msanii huyo amedai kuwa kutokana na yeye kuwa na mahusiano mazuri na uongozi, basi chuki zilianza kiasi cha kusababisha ugomvi wa mara kwa mara.

Anasema alitakiwa aendelee kuwepo kwenye kikundi hicho hadi Februari mwakani, lakini ameona bora atoke mapema.
Jitihada za kuzungumza na viongozi wa kundi lake zimegonga mwamba kwani hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kufafanua suala hilo.

Sunday, December 4, 2011

AMBASSADORS OF CHRIST KUFANYA KWELI LEO...


KUNDI la Muziki wa Injili la Ambassador of Christ kutoka Rwanda limetua na kuahidi kushusha shoo ya nguvu LEO Jumapili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa albamu yao ya'Dukwie Gushima' ikiwa na maana ya Twapita Kushukuru.

Albamu hiyo ni mpya baada ya ajali iliyoua wasanii watatu wa kundi hilo; Filbert, Ephraem na Amos iliyotokea Kahama, Shinyanga Mei mwaka huu wakati kundi hilo likirudi mjini Kigali baada ya kutoka Dar es Salaam.

Albamu hiyo ina nyimbo 11, lakini watatumbuiza pia kwa nyimbo za 'Kwetu Pazuri', 'Kazi Tufanye' na nyinginezo.
Kundi hilo ambalo limejipatia umaarufu mkubwa hususani ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuimba nyimbo kwakutumia kutumia lugha fasaha ya Kiswahili,lilitua jijini Dar es Salaam jana Ijumaa likiwa na waimbaji 33. 


Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kulakiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa muziki huo, mwalimu wa kwaya wa kundi hilo,Sozzy Joram alisema;

Tumeamua kurudi Tanzania kuja kuzindua albam yetu kwavile ni nchi yenye watu wakarimu,tulikuwa pamoja wakati tulipopata ajali na wenzetu watatu wakafariki.

Kitu ninachoweza kuwaahidi ndugu zetu Watanzania waje kwa wingi Jumapili kwa pamoja tumsifu Mungu kwa kutuepusha na ajali mbaya kwavile tungeweza kufa wote,"alisema Joram. 

WAKURUGENZI WA TFDA WATUNUKIWA VYETI...

Mshauri wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Legu Mhangwa  akimtunu cheti cha Umiliki katika Uongozi  Adam Fimbo , jijini Dar es salaam. 

Zaidi ya wakurugenzi na meneja 500 kutoka katika taasisi na mashirika zaidi ya 30 nchini wametunukiwa vyeti vya mafunzo ya uongozi kutoka katika taasisi ya Crest Business Trainers.
Kati ya wahitimu hao mwishoni mwa wiki hii meneja na wakurungezi 10 kutoka mamlaka la dawa na chakula (TFDA) walitunukiwa vyeti vya mafunzo ya jaketi la uhimili katika uongozi .
Mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na Crest Business trainers ambao ni wakala wa Crestcom international kutoka nchini marekani yalikuwa ni mafunzo ya siku tano.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya viongozi hao kutunukiwa vyeti,  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Bi Hafsa Mahinya alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kubadilisha mtazamo wa viongozi wa mashirika hasa katika kuboresha utendaji wao wa kazi.
Alisema kuwa mafunzo hayo hutoa elimu katika nyanja mbali mbali katika kuhakikisha utendaji wa kazi wa viongozi hawa unaboreshwa na kuweza kukidhi haja ya mhudumiwa na hata kukidhi haja ya kampuni ama shirika analofanyia kazi.
“Haya ni mahafali ya tisa tangu tumeanza kutoa mafunzo haya na tumeona mafanikio makubwa kwa wahitimu wote waliopata mafunzo haya na asilimia kubwa ya wahitimu wamepanda vyeo kutokana na utendaji wao wa kazi kuboreshwa,” alisema.
Alisema kuwa Meneja wengi hawana muda wa kuwa nao kwa muda wote hivyo wameamua kutenga muda wa saa 48 kwa siku tano ili kuweza kuwapata na kuwapatia mafunzo hayo.
Aliongeza kuwa kati ya mashirika ambayo yaliwahi kunufaika na mafunzo hayo ni pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao walipatiwa mafunzo hayo kwa mara 2 mfurulizo, shirika la mawasiliano ya simu Tanzania (TTCL) ambao wakurugenzi wake wamepatiwa mafunzo yaho mara 4, na kampuni ya simu za mkononi airtel ambayo imepatiwa mafunzo hayo mara 2.
Alisema kuwa mafunzo hayo yenye lengo la  kubadilisha mtazamo wa vingozi hawa ili waende na taratibu za kufanya biashara na aliongeza kuwa mafunzo hayo yalianza kutolewa katika taasisi na mashirika mbali mbali tangu mwaka 2002.
Naye mshauri wa tiba na dawa kutoka TFDA Mr Legu Mhangwa alisema kuwa mafunzo haya yatawawezesha viongozi hawa kuweza kupata matokeo mazuri hasa katika suala zima la kubadilisha mtazamo.
Alisema kuwa ni kazi ya mamlaka kufundisha wafanyakazi ili waweze kutoa huduma bora kwa wanaopokea huduma hizo ambao ni jamii kwa ujumla.