BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, July 17, 2010

1. izo ni za kwapa za apo down itakua balaa
2. duuuuuuuu dada huyu kabarikiwa, wakati huku bongo tunaangaika na weaving mwezetu kwapa limejaa!sipati picha makaomakuu itakuwa vp!-happy-morogoro
3. NI MZURI ILA ANABONGE LA AFRO KWAPANI a.k.a SOUTH AFRICA:-Phily 4life.
4. UWE UNANYOA HIZO NYWELE HAMNA ANAETAKA KUANGALIA.BY-K.K. MWANZA
5. Chawa wa kidhungu wanamuwashawasha
6. duh hii ndio kwapa chini kukoje?by ya4 FR
7. Hizi fesheni zingine bwana...,sasa hawa dada zetu vigi za makwapani watazitolea wapi? - SK
8. unaweza ukajifichaa,kariakoo

Kupitia Sibuka Fm Sauti ya Jamii ya Afrika ya Mashariki katika masafa ya Satelite katika audio 4 right katika TBC1 television, Fm kwa 94.0 kwa Pwani na Dar, 104.9 kwa Shinyanga na pande za maswa kupitia 97.0 inasikika....!

Moja vijimambo vilivyojili katika wiki hii ndani ya sibuka fm radio!
Juma Bakari kazomba( JB) ndani ya nyumba!

Mrembo Anna Shoo member wa TSJ naye yumo!

Hapo chacha Jembe aka Omary Said na yeye hapitwi wiki hii...!


Daah! wa ukweli Halima Kambi.

Hapo ndani ya mjengoni napiga kazi Mkesha wa kazi baaaaby!!!!

Jembe naye huyo mkeshani!

One Love to all blog viewers wangu au sio tuko pamoja na kumbuka kutune frequence hizo pale kati braaaaaaah braaaaaaaaah utakwenda na maji!!!!!!!

Ni mwendo wa DESPARADO!

Baada kimya cha muda sasa,mwanadada Baby Madaha,ambaye pia ni chimbuko la Bongo Star Search (BSS) hivi karibuni amerelease single mpya aliyoipa jina DESPERADO...kazi ikiwa chini ya Producer Allan Mapigo.



Kwa mujibu ya mrembo huyu,single hiyo itakuwa moja ya track zilizomo ndani ya sound track ya kampuni la PILIPILI INTERTAINMENT ambayo itaitwa OBSESSION.

Alipoulizwa wimbo Desparado unazungumzia nini haswa,mwadada huyu alisema....
"Kwanza watu wataipenda kwasababu nimeimba kuhusu upande wa pili wa Mapenzi, unampenda mtu na unampa yote halafu tena hakujali, matokeo yake napata mwingine halafu yeye anarudi tena, hapo ndo ndipo ishu inapokuwa nzito." alimalizia fashionista huyo.

Friday, July 16, 2010

BIFU YA KIDUM NA HERMY B: UKWELI ULIOFICHIKA KUHUSU WIMBO WA NITAFANYA KIDUM FT LADY JAYDEE





habari hii inatoka kwa mdau kutoka Bongo5.com 


Hivi karibuni kulitokea kutoelewana kati ya Producer Hermy B na masanii aliyekuja kwa kasi Kidum. Bongo5 iliamua kumtafuta Hermy B hili kuzungumzia nini chanzo cha Beef Yao. na Hermy hakusita kunitumia Email na kuelezea kila kitu.
Email kutoka B Hits...
Ngoja nitoe ukweli wa huu wimbo.

Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy ambae alikutana nae project fame kule Nairobi. Wakakutana na kufanya kazi pamoja..katika maana ya kwamba mziki huu uliundwa na Hermy na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern Yoote ni Ya hermy.
Kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na Rkay(jamaa anaetengeneza mziki wa Wahu examples sweetlove, runin low) madhumuni ni kutengeneza video ya wimbo huu. Cha ajabu Rkay akamtengeneza kidum mpaka akakubali kurekodi upyaa wimbo huo. Rkay alikopi kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, ila kisheria alibeba Idea ya kisanii ya Hermy kama ilivo. yote haya yalifanyika bila kuomba ruhusa wala kumpa taarifa Hermy.
Muda ulipofika Hermy alitoa huo mziki kwa radio stesheni, na kidumu alikimbilia kuomba wasiucheze huo wasubiri ule wa Rkay..alipoulizwa huu una tatizo lipi alishindwa kujieleza na akagundulika hana mantiki zaidi ya Ubaguzi wa sanaa tu. Stesheni flani flani wakakubali kuupokea na kuucheza huu wa kwetu Tanzania. Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa Rkay ukichezwa na upo kwa video aliyopiga Rkay kwa sasa. Mwenye maskio na aliyeskia wimbo huu mara ya kwanza atajua tu huu uliopo kwenye video ni tofauti na vyombo vimepunguzwa, sio kwamba Rkay hajui kutengeneza muziki, ila alikua akijaribu kujitofautisha sana na Hermy na amejikuta akiharibu kiasi flani sanaa hiyo. Ninachoomba ni kwamba watanzania tuendelee kushikamana na kupeana suport kwenye wizi wa sanaa kama huu. Tuwe na cha kujivunia kwa watengeneza mziki wetu. Asalaamu!

PICHA ZA KIDUM NA HERMY USIKU WA KUREKODI WIMBO WA NITAFANYA



Wednesday, July 14, 2010

Ndoa ya Christina Milian na The Dream yavunjika Kimya Kimya.!

Christina Milian na The Dream

Msanii Christina Millan na mume wake ambae ni mwimbaji/ mtaarishaji wa muziki na mwandishiwa nyimbo vilevile namzungumzia The Dream wameamua kutemana. Terius Nash a.k.a The Dream, ametoa taarifa hizo kwa mtandao wa UsMagazine.com, ambapo mtandao huo umeandika kuwa The Dream anasikitika kutangaza kuwa ndoa yake na Christina Milian haikufanikiwa, yaani imevunjika,




Wawili hawa walifikia hatua hii mwishoni mwa mwaka 2009, laikni waliamua kutokutoa taarifa hizo ili isije kumuathiri mtoto wao wa kike Violet, The Dream ameamua kutoa taarifa hizo kutokana na picha alizopigwa akiwa na msaidizi wake anayeitwa Melissa Santiago, picha hizo walipigwa wakiwa katika visiwa vya Caribbean, so watu wakahoji iweje mchizi aonekana na dem mwingine wakati ana wife? Dream akaona bora afunguke kuliko kuacha Funs wake wamuone yeye ni Play boy.

RIHANNA AZUNGUMZA NA EX BOY WAKE CHRISS BROWN!

 RIHANNA

Msanii wa muziki wa nchini marekani Rihanna azungumza na ex boy wake chris brown baada ya kutazama show kali aliyofanya Chris katika utoaji wa tuzo za wasanii bora nchini marekani, za BET 2010 awards.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa Rihanna alioneka kupatwa na hisia na kufurahishwa na show hiyo aliyofanya msanii huyo aki perfome kwa hisia wimbo wa michael jackson wa "thriller", Rihanna asema kuwa hajawahi kumuona Chris akifanya hivyo hapo awali hivyo aliguswa na kumuona alivyokuwa.

Naye Chris alisema kuwa anajihisi kama sasa hivi anajiona amekua baada ya mwaka mmoja huo waliokuwa wametengana. Alisema kuwa nafuraha sana kuwa in touch na Rihanna.

CHRIS BROWN

Wapenzi hao wawili hawajazungumza karibu kwa mwaka mzima tangu Chris Brown alipotuhumiwa kwa kumpiga Rihanna Vibaya..!Sasa wamekuwa wakichat kwa kutumiana ujumbe mfupi pia wakiwa na plani ya kuja kuonana uso kwa uso ingawa kuna masharti ambayo Brown alikuwa amepewa,kuwa lazima awe umbali na Rihanna wa yard 100 kwa muda wa miaka mitano. duuh bonge la adhabu kwa umpendae!!

Suala la kujiuliza kuwa jee wanataka kurudiana nini??!