BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, October 29, 2011

TAO AVULIWA UNGOZI WA UNAIBU KATIBU MKUU LEO..

VURUGU kubwa zilitokea jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano Mkuu wa  Halmashauri kuu ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), wakati wa kujadili rufani iliyowasilishwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Hamad Tao kupinga kusimamishwa kwake.
Kutokuelewana huko kati ya mwenyekiti wa TLP, Dk. Augustino Mrema,wanachama na Tao wakati akiwasilisha rufani hiyo ambapo licha ya kupewa mda kujitetea ndipo alipoanza kujadili kiti ambacho hakukieleza katika rufani hiyo.
“Tao unatakiwa kueleza kile ambacho umekiwasilisha kwa njia ya maandishi na sio kama unavyo fanya kuongea ambayo hukuyawasilisha,”alisema Victor Limo Katibu Mipango wa TLP.

Hata hivyo Tao aliendelea kueleza kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya TLP ambapo alidai ndio sababu ya yeye kuenguliwa na mkutano mkuu wa chama kwa kudai kujua.
“Chama chetu kinaendeshwa kidikiteta na mwenyekiti watu,hata ukitaka kujua mapato na matumizi huwezi pata nah ii nduio sababu ya nyinyi (wajumbe) kunitoa mimi katika uongozi lakini nawahakikishia kuwa mtawafukuza wengi kwa hili,” alisema Tao.
Baada ya kauli hiyo ndipo mabaunsa wa TLP waliokuwapo katika ukumbi huo kumtoa kwa nguvu huku ukumbi wote ukizizima makelele kuashiria kikomo cha uongozi wa Tao.
Kwa upande wake Dk. Mrema alisema kuwa Tao amekuwa akikiyumbisha chama kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kuwaachia wengine kukiongoza ambao watakuwa na uchungu na maendeleo ya TLP.
“Nawaomba wanachama kutupilia mbali rufani ya Tao kwni amekiingiza chama katika migogoro na kukirudisha nyuma kwa kipindi kirefu sasa na umefika wakati way eye kuwa mwanachama tu na sio tena kiongozi kwani anaonekana kuwa anatumiwa na watu kutuweka hapa tulipo sasa,”alisema Dk. Mrema
Dk. Mrema aliongeza “Kwa kuwa mimi ndiye niliyemteua Tao kuwa naibu katibu mkuu hivyo basi namamlaka ya kumuondoa nyadhifa hiyo na kama atataka asubiri uchaguzi mkuu mwaka 2014 naye agombee kwa juhudi zake na kama atashinda ndio atuongoze lakini kwa sasa utupishe”.





Friday, October 28, 2011

MPIGIE KURA SALHIM SHAO..

wadau wa blog hii napenda kuwaarifu kuwa mdau mwenzetu salhim Shao Mpiga picha kutoka gazeti la The Citizen, mwananchi na mwanaspoti ameteuliwa kuwa mmoja wa wanaowania tuzo za mpiga picha bora za mitindo Tanzania kupitia shindano la Swahili week fashion show awards, shindano ambalo linaratibiwa na Swahili fashion week chini ya Mustafa hasanali.
Wito wangu kwenu ni kushiriki kumpigia kura kupitia www.swahilifashionweekawards.blogspot.com naamini tutafanya hivyo kuhakikisha anapiga hatua.
Thanx wadau

REDDS UNI-FASHION BASH KUFANYIKA KESHO CHUO KIKUU..

Wa kwanza kulia  ni Meneja wa Redds Bi Vick Kimaro akifuatiwa na mmoja wa washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja wakizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.
Wa kwanza kushoto  ni Meneja wa Redds Bi Vick Kimaro akifuatiwa na washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja kutoka chuo cha CBE akifuatiwa na Aloycia Innocent (UDSM) na wa mwisho kulia ni Asha Mohamed (KIU) wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.
Washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja kutoka chuo cha CBE wa kwanza kulia akifuatiwa na Aloycia Innocent (UDSM) na wa mwisho kushoto ni Asha Mohamed (KIU) katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.

WABUNIFU wa mavazi wapatao 18 na wanamitindo 24 kutoka vyuo mbali mbali jijini Dar es Salaam leo watashiriki katika onyesho la mavazi lijulikanalo kama Redd’s Uni-fashion Bash lilipangwa kufanyika katika ukumbi wa FPA katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Onesho hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original limeghalimu kiasi cha shilingi million 100 katika maandalizi pamoja na zawadi za washiriki kwa nchi nzima.
Tamasha hili litashirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyo katika mikoa minne ambapo Dar Es Salaam ni mkoa wa kwanza ikifuatiwa na Kilimanjaro, Dodoma na Mwanza.
Akizungumza katika uzinduzi wa fainali za onesho hilo kwa Dar es Salaam, meneja wa Kinywaji cha Redd’s Bi Victoria Kimaro alisema kuwa tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo kupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo.
 “Wanafunzi hawa wenye vipaji vya ubunifu wamepata fursa ya kuonesha ubunifu wao wa mitindo na hii ni fursa kubwa sana kwao kujitangaza na kudhihirisha uwezo wao,” Bi Kimaro aliongeza.
Bi Kimaro alisema zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hawa ili waweze kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za pesa taslim washindi watano katika kila mkoa watakaoshika nafasi za juu.
Alisema kuwa wabunifu wa mitindo watakao shika nafasi ya kwanza watapatiwa kitita cha Sh 700,000, mshindi wa pili 500,000        na mshindi wa tatu atapaitiwa Sh 300,000 pia mshindi wan ne na wa tano watapatiwa Sh 100,000 kila mmoja.          
Aliongeza kuwa wanamitindo watapatiwa Shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza na wa pili atapatiwa Shilingi laki nne akifatiwa na wa tatu ambaye atapatiwa shilingi laki tatu na washindi wa nafasi ya nne na tano  watapatiwa laki moja kila mmoja.
“Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia tamasha hili litahusisha burudani mbalimbali za kuvutia kutoka kwa wasanii wa bongo flava ambao ni Roma Mkatoliki na Joh makini na pia hii ni sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali katika kufurahia na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya ubunifu na mitindo,” alisema.
Aliwataja washiriki wa onesho hilo kuwa ni Aloycia Innocent kutoka USSM, Rosemary Osward (CBE), Magreth mhoza (MNMA) Upendo Kuboja (CBE) na Kudra Lupatu kutoka CBE.
Wengine ni Emmanuel Elly kutoka CBE, Lameck Stephen (IFM), Benson Macha (CBE), Saadat Juma (IFM) Conrad Gumbo (IFM), Issack Ibrahim (UDSM), Amos Kalinga (UDSM) na Asha Mohamed kutoka KIU.
Washiriki wengine saba ni Rose Hubert kutoka KIU, Gerald Kalinga (UDSM), Hussein kasim (UDSM), happiness Mushi (CBE), Yalita Malanduzi (UDSM), Brian Abdul (CBE) na Rosa Damazo(IFM)
Bi kimaro pia aliwataja majaji wa tamasha hilo kuwa ni Taji Liundi, Hamisa Hassan, farouk Abdala na Castantine Magavile.