MSANII wa muziki nchini Mrisho Feruzi a.k.a Feruzi amesema kimya kingi kina mshindo mzito na kwamba anajipanga kikamilifu ili albamu yake iweze kukubalika.
Feruzi ambaye alikubaliaka sana katika tasnia ya muziki miaka ya nyuma kupitia wimbo wake wa Starehe anasema hajafulia kimziki na kuwa bado yupo kwenye game.
“Muziki ni kazi kama ilivyo kazi nyingine lazima ujipange ili uweze kutoa ujumbe wenye ladha kwa mashabiki waliokuzoea na wasiokuzoea,” anasema.
Anasema ukimya wake utakuwa na manufaa kwa muziki wa bongo hasa ukilinganisha na aina ya muziki na kwamba bado kitambo kidogo atavunja ukimya huo.