Alianza kuimba kabla ya kushiriki katika mashindano ya Tusker Project Fame Season 4, Prudence Kibaya ni mmoja wa wasanii chipukizi ambao maisha yao ya kimuziki yanatarajiwa kuwa bora zaidi siku za usoni.
Baada ya kushiriki kwenye mashindano hayo ya TPF4, mwanamuziki huyo chipukizi alitoa kibao kiitwacho 'Nataka Cheza' akimshirikisha mwanamuziki maarufu wa mjini Mombasa aitwaye Labalaa.
Licha ya kuwa alikuwa anapenda kuimba, Prudence alijitosa katika dunia ya muziki miaka miwili iliyopita akiwasaidia wasanii wengine katika studio za kurekodia muziki.
Katika kipindi hicho, Prudence pia alifanya 'kolabo' na msanii wa Mombasa, Husler J katika wimbo uitwayo 'Minyororo ya Haki'.
Kwa sasa wakati kibao chake kipya kiitwacho 'Shuka' kinavuma nchini, Prudence anakubali kuwa fursa aliyoipata ndani ya TPF4 ilimpatia mafunzo mengi kuhusu muziki.
Akiwa mwanafuzi wa taaluma ya habari katika Chuo Kikuu cha Mombasa Polytechnic, Prudence anasema kuwa anatayarisha albamu ambayo ananuia kuizindua mwishoni mwa mwaka.
Ingawa alizindua kibao 'Shuka', mwanamuziki huyo chipukizi anasema kuwa yuko na vibao vingine ambavyo kwa sasa viko studioni. Kwa sasa, anasema, tayari ana mkataba wa kurekodi nyimbo tano na Grandpa Records huku akiongeza kwamba anajiandaa kufanya 'kolabo' na mwanamuziki mwingine maarufu Afrika Mashariki, Nyota Ndogo.
Prudence anasema kuwa anaweza kufanya shoo za muziki katika sehemu yeyote nchini wakati wowote atakapohitajika, lakini akaongeza kwamba anafarijika kutokana na maoni mengi anayoyapata kutoka kwa mashabiki wake kupitia mtandao wa internet.
Akaongeza kwamba ananuia kuanzisha bendi yake mwenyewe ya muziki ambayo itawahusisha wasichana peke yao na kuwa na matumaini kwamba huenda akaweka rekodi ya kuwa na kikundi cha wasichana pekee kitakachokuwa maarufu na kutoa burudani.
“AFRICAN BEAUTY” IS JUST ANOTHER ONE FROM DIAMOND PLATNUMZ & OMARION WHICH
MIGHT BE THE JAM OF THE CONTINENT
-
The Tanzania Recording Artist Diamond Platnumz released “African
Beauty” off his just premiered album “A Boy From Tandale”. The album
features Top Artist...
6 years ago