BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, March 26, 2012

ANZISHA PRIZE KUWANUFAISHA VIJANA WAJASILIAMALI WA KITANZANIA...

Mkurugenzi wa African Leadership Academy, Jamila Payne (Kushoto) akizungumza na Wanafinzi kutoka Shule mbalimbali za jiji la Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa kujadili mladi wa Anzisha Prize wakishirikiana na Tume ya Sayansi  na Teknolojia Tanzania katika kutafuta vijana wenye ubunifu katika kuanzisha miradi ya ujasiriamali.

Mkurugenzi wa African Leadership Academy, Jamila Payne (Kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa mpango wa Anzisha Prize wakishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania katika kutafuta vijana wenye ubunifu katika kuanzisha miradi ya ujasiriamali hasa kwa wanafunzi wa shule za sekondari na Vyuoni
Mshindi wa nne katika shindano la Anzisha Price 2011, Fredrick Swai (Kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa vyuo mbalimbali walihudhuria mkutano wa kujadili mradi wa Anzisha Prize wakishilikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania kuendesha shindano la kutafuta vijana wenye ubunifu hasa katika kuleta mapinduzi ya teknolojia

TUME ya Sayansi na Tekinolojia Tanzania (Costech) kwa kushirikiano na African Leadreship Acadeemy (ALA) ya Afrika ya Kusini  wameamua kuinua vijana wa hapa nchini kwa walio na ubunifu wa kisayansi ili kuweza kujenga uwezo vijana kumudu na kuzitatua changamoto mbalimbali za kijamii.

Kupitia tuzo za Anzisha prize ambazo zilianzishwa mwaka jana na kuhusisha nchi zaidi ya 23 barani Africa itawawezesha vijana kutoa mawazo yao kwa kufanya vitu mbalimbali vitakavyo weza kutatua matatizo katika jamii.
Akizungumza na wandishi wa habari  jana Mkurugezi wa habari na nyaraka kutoka COSTECH Raphael Mmasi alisema kuwa vijana wengi wa kitanzania wana ndoto japokuwa hawana pakuwezesha ndoto hizo, na  kutokana na pato la nchi kuwa  dogo na kutofikia malengo inachangia vijana wengi kujiingiza kwenye mambo yanayosababisha wengi kupoteza ndoto zao
“Tumeanzisha mpango huu kwa makusudi ya vijana wa Afrika nzima kutimiza ndoto zao zisipotee bure na moja ya majukumu yetu ni kuibua vipaji vya Sayansi”alisema Mmasi.
Alisema kuwa mradi huo utahusisha vijana wenye umri wa miaka15 mpaka20 ambao wameweza kubuni kitu chochote kinachoweza kutatatua changamoto zinazoikumba  jamii inayomzunguka.
Alisema kuwa mwaka jana walifanya shindano hilo na  Joel Mwale kutoka Kenya alikuwa mshindi wa kwanza, mwaka huu mshindi wa kwanza atapatiwa dola elfu75 kama zawadi na  mashindano yatafanyika hivi karibuni nchini Afrika ya kusini.
Bw Mmasi alisema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanategemea umeme unaozalishwa na maji, hivyo kupitia mawazo mbalimbali yatakayotolewa na vijana hawa yataweza kutatua kero hiyo na kupendekeza njia mbadala za kuzalisha umeme mfano kupitia jua na rasilimali zingine.
Fredirick swai(20) ambaye ni mshiriki wa shindano hilo la mwaka2011 kutoka Tanzania  alisema kuwa kwa mwaka huu wanatarajia kupata maombi mengi zaidi kuliko mwaka jana maombi yalikuwa 180 kutoka nchi 23 za Afrika.
Katika walsha iliyo fanyika jana walipokea wanafunzi 70 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kwa siku ya leo wanatarajia kutembelea shule ya sekondari oyersterbay kutoa elimu ya kutosha  juu ya umuhimu wa tuzo hizo.