BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, May 16, 2011

Msanii SANGALO apania kutoka kikamilifu.


Na. FRANK AMAN.

Sangalo mtoto wa mzee mashaka(Mr Mzinda) katika filamu ya Masaa Matatu (3 Hours) ameonesha na kudhihilisha kipaji chake vema  katika tasnia ya filamu Tanzania.

Hivi karibuni Kabumbu lilifanya mazungumzo na kijana huyu nayo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mwandishi: Jina lako kamili ni nani na ulizaliwa mwaka gain?

Sangalo: JohnVicent Sangawe, nimezaliwa mwaka 1987 mkoani Kilimanjaro.

Mwandishi: Elimu yako umepatia shule gain?

Sangalo: Elimu ya msingi nimesomea shule ya msingi Kimara na nikajiunga na           Sekondari ya ubungo modern ambapo nimehitimu mwaka 2009.

Mwandishi: Ulianza lini mambo ya sanaa ya kuigiza?

Sangalo: ulikuwa ni mwaka 2006 baada ya wazazi  wangu kufariki mwaka 2004,    niliwaza na kuwazua nikaona ni lazima nianze kutengeneza maisha kidato  cha kwanza, nikajiunga na kundi la Christian Promotion ambalo siku hizi hadi ndipo nikaendelea nafasi yangu ya kuigiza.

Mwandishi: Baada ya hapo utahamia kundi gani/ kampuni gani?

Sangalo:  Nilijiunga na MOJA FILM ENTERTAINMENT hapo mwaka 2010 kampuni ambapo bado mnafanya kazi mpaka sasa.

Mwandishi: Mbali na kucheza kama motto wa mzee Mashaka katika filamu ya Masaa matatu  umewahi kushiriki filamu ingine yoyote?

Sangalo: Ndio, nilicheza  nafasi ya mhudumu wa bar katika filamu ya My Pastor mwaka 2007 na mwaka 2008 niliigiza mwanafunzi wa shule ya msingi katika dangerous girl.

Mwandishi: Unatarajia nini badae?

Sangalo: Kuwa msanii bora wa filamu Tanzania na duniani.

Mwandishi: Unatarajia nini kutoka kwa wadau wa filamu?

Sangalo: nataka sapoti ya hali na mali ili nisimame mwenyewe kwa miguu miwili, ikiwezekana niendeshe shughuli zangu na kuishi kwangu, kwani sasa naishi Kimara kwa kaka.

Sangalo: Namshukuru mungu, ndugu zangu, marafiki na kiongozi wa moja film.