BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Friday, December 10, 2010

STEP UP PREYER BEACH PARTY.

Bonge la party litakalo fanyika pande za mbalamwezi Beach club Mikocheni siku ya alhamisi tarehe 23 december 2010. Show hii iko powered na Clouds TV kupitia kipindi cha step up prayaz... Bata za beach party utazipata kwa buku 5 au buku 7 mlangoni.

Wednesday, December 8, 2010

PETER MSECHU AWASILI NYUMBANI-TZ

peter msuchu akirajea nchini.

 moja ya shamla shamla za kumpokea.
fuuull happy being back home..

 wecome back peter.


Akiwa katika pozi home..

Karibu sana msechu kutokja huko kenya katika mashindano ya Tusker project fame ki ukweli umetuwakilisha vizuri Tanzania tunaamini umefungua njia kwa watanzania wengine kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa session zinazofuata..  tha zealot

Monday, December 6, 2010

AMPLIFIER SHOW MPYA KUTOKA KWA MILLARD AYO CLOUDS FM.


LEO katika pita pita zangu katika kusikiliza Radio za hapa kwetu TZ nimepata nafasi ku tune katika 88.4 Clouds Fm peoples station mida ya saa moja hivi na nimepata kusikia sauti ya mtangazaji ambaye nilikuwa nimemiss kwa muda sauti yake, anafahamika kama MILLARD AYO  aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Radio cha Radio 1 stereo hivi sasa ni mwajiriwa  mtangazaji wa kituo cha  radio cha Clouds fm na leo alikuwa katika show yake mpya ya AMPLIFIER ambayo imeshika nafasi ya kipindi cha BAMBATAA kilichokuwa kikiongozzwa na mwanadada Sofia Kessy hivi sasa hakitakuwepo tena na badala yake wapenzi wa station hii tutapata nafasi ya kusilia kipindi hiki cha Millard kila siku za wiki kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku j3 hadi ijumaa.



Kijana huyu amekuja kivingine kabisa na show yake ni bonge la show zaidi ya ile aliyokuwa nayo Radio nayo ya Milzo 101.Pia kuanzia January 2011 atakuwa na show yake mpya kupitia kitua cha televisinon cha Clouds TV.

Sunday, December 5, 2010

DAVIS NTARE AJISHINDIA MIL.5 KSHS TUSKER PROJECT FAME 4.

Mshiriki DAVIS HILLARY NTARE aliyeshiriki mashindano ya kuibua vipaji vya uimbaji hapa Afrika ya mashariki na kati la TUSKER PROJECT FAME, ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambacho kinahusisha nchi sita kutoka Afrika Mashariki. Davis amejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 5 za kenya. 

Hii ni mara ya pili kwa nchi ya Uganda kunyakua ushindi huo, kwa mara ya kwanza katika Tusker Project Fame season 2 ushindi ulichukuliwa na Esther Nabaasa, na PTF3 ushindi ulikwenda kwa Alpha kutoka nchini Rwanda ambaye pia aliibuka tena mshindi katika tuzo za PAM akiwa kama PAM best artiste from Rwanda.

TANZANIA ikiwa kama washiriki katika shindano hilo imeweza kushika nafasi ya pili ikiwakilishwa na PETER MSECHU, nafasi ya tatu imeshikwa na STEVEN kutoka Kenya na nafasi ya nne ikiwa imeshikwa na AMILEENa kutoka Kenya pia.
Nampongeza sana Devis kwa ushindi huo, pia Msechu kwa kuweza kufika nafasi hiyo kubwa ambayo Tanzania hatujawahi ifika kwa mashindano hayo, pia nampongeza kwa kuweza kuiwakilisha Tanzania ipasavyo, bila kuwasau washiriki wengine kutoka Tanzania, Leah Moud, Aneth,na Cynthia ki ukweli wamejitahidi sana.

Changamoto kwa watanzania wenzangu jamani tushiriki kikamilifu katika kuwasappoti wenzetu wanapokuwa katika mashindano hayo ili na sisi siku moja tuweze kunyakua ushindi huo. Tujitolee kuwapigia kura washiriki kwa kila tuwezavyo kwani kilichomwangusha Msechu ni kura na sio suala la uimbaji..