BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Thursday, September 16, 2010

DIPLOMA WA TSJ WASHEREKEA BASH NA KILIO CHA MABAO 3 KUTOKA ACC KWENYE MECHI YA KIRAFIKI.


Timu ya Wanafunzi wa Diploma Tsj.

WANAFUNZI Chuo cha uandishi wa habari  cha Time school of journalism(TSJ), jana walikuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu baina ya wanafunzi wa A-stashahada (certificate) na Diploma (stashahada) na wanafunzi wa Certificate waliibuka washindi kwa kuwafunga Diploma kwa mabao 3 kwa 2 kwenye mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa garden maeneo ya Ilala Bungoni jijini Dar es salaam.

Timu ya Wanafunzi wa ACC TSJ

Wakizungumza na blog hii baadhi ya wachezaji walisema kuwa mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki na imejenga umoja na muendelezo wa mazoezi kwa chuo chao kutokana na utani wa jadi uliokuweko baina ya wanafunzi hao ambao wanasomea kozi ya uandishi wa habari katika ngazi tofauti ikiwa ni Certificate na Diploma.
Hata hivyo waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho (TISJOSO) ameongeza kuwa mechi hiyo ilifanyika kwa amani bila ya kuwa na ugomvi na malumbano ya hapa na pale na pia akawasititiza wanafunzi kuendelea na moyo huo huo wa kujijenga kimichezo ili waweze kucheza mechi tofauti tofauti na vyuo vingine.

Wakiwa uwanjani.

MBALI na hilo pia chuo cha Time School of Journalism (TSJ) kupitia serikali ya wanafunzi ya chuo hicho wameandaa BASH ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa ngazi hizo mbili za certificate na Diploma inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Cine Club siku ya Jmosi tarehe 18 mwezi wa 9/ 2010.

Kulia ni Miss Tsj Lilian Andrew na Katika ni Benadina Mwita miss no 2 na kushoto ni Somoe Nkomoe mwanafunzi TSJ.

Na akizungumzia maandalizi ya sherehe hiyo waziri wa michezo wa chuo hicho amesema kuwa  itakuwa ni bash ya kihistoria na ina muchezo lukuki itakayofanyika hivyo amewasihi wanafunzi kujitokeza katika bash hiyo ili kujifunza na pia kujenga mahusiano mazuri na wanafunzi wenzao wapya. michezo ambayo itakuwepo katika Bash hiyo ni Miss na Mr TSJ, Vichekesho, Maigizo, Kuimba, Kukimbia na gunia, mashindano  ya kunywa soda na michezo mingine mingi, na pia amewaaalifu kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo ni Mhesimiwa IDD AZAR ZUNGU mbunge wa jimbo la Ilala na wageni wengi waalikwa.

Thazealottz inawatakia sherehe njema wanafunzi wa chuo cha TSJ na washerekee kwa amani na maadili.

Sunday, September 12, 2010

Mambo manne ya kuzingatia Kama unataka kuacha/kupunguza pombe!



Pombe ni burudani, huondoa uchovu na kuchangamsha mwili, lakini wakati mwingine pombe ikimzidi mtu huweza kumharibia hata mipango mbalimbali ya maisha yake. Hapo sasa ndipo shauku ya mtu kutaka kuacha pombe inakuja.

Hata hivyo, pamoja na shauku hiyo ya kuacha pombe, wengi hushindwa kutokana na mwili wake kuwa tayari umeshazoea pombe. Hapa nitakupa njia za kitaalamu kabisa ambazo ikiwa utazitumia kwa umakini, inaweza kuwa rahisi sana kwako wewe mlevi kupunguza kama siyo kuacha kabisa kunywa pombe.

Sasa soma mtiririko ufuatao.

KIMBIA KAMPANI ZA POMBE
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo unatakiwa kuifanya wewe ambaye una nia ya kupunguza au kuacha kabisa kunywa pombe. Achana na marafiki zako walevi, usipende kufanya vikao katika baa au kumbi za starehe.

TAFUTA VITU VYA KUFANYA
Wahi kufika nyumbani, na tafuta vitu vingine vya kufanya kama kusoma magazeti, kuangalia filamu na mengine mengi ya kupendeza. Ni rahisi tu kufanya hivyo. Kwanza uanweza ukabadilisha ratiba yako ya kazini. Jiongezee ubize kwa kadri uwezavyo, ili utakavyotoka kazini uwe mchovu, unayewaza maji ya kuoga na kupumzika huku ukipata burudani nyingine kama nilivyoeleza hapo juu.

BADILI VINYWAJI
Kwakweli ni vigumu sana kuacha pombe, lakini kama una nia ni rahisi pia. Pindi uhisipo hamu ya kunywa pombe, tumia muda huo kunywa chai, kahawa, juisi au maziwa. Kwa kawaida, baada ya kunywa vinywaji vya baridi au moto vyenye sukari, hukata au kupunguza hamu ya kunywa pombe.

AMUA KWA DHATI
Pamoja na yote hayo niliyoyafafanua hapo juu, ni jukumu lako wewe na moyo wako kuamua kwa dhati kabisa kwamba “SASA HUTAKI TENA KUNYWA POMBE! Ikiwa utakuwa na imani hii moyoni mwako, ni rahisi sana kuacha pombe.