SERIKALI ya wanafunzi ya chuo cha uandishi wa habari
cha Time School of Journalism (TSJ) inatarajia kuwapata wawakilishi wapya wa
taji la Miss na Mr TSJ katika sherehe za ‘Bash’
ambazo zimelenga kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza katika
chuo hicho.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa
kufanyika mwishoni mwa mwezi August tarehe 25 zitafanyika katika uwanja wa
Mwalamwezi Beach, na itasindikizwa na wasanii mabli mbali wa muziki wa Bongo
flava.
Akizungumza na gazeti hili, Rais
wa chuo hicho Bi Frida Matinya alisema kuwa sherehe hizo ni moja ya utaratibu
waliojiwekea katika kuwapokea wanafunzi wapya ambao ni wameingia chuoni hapo
kuchukua kozi mabli mbali.
Alisema kuwa katika sherehe hizo
ambazo zitashereheshwa na michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya
mavazi, Mr na Miss TSJ, Kuimba, kuvuta kamba, kuogelea na michezo mingine mingi
ya baharini.
“Lengo la sherehe hizo ni kuwa
kawaweka karibu wanafunzi wageni na pia kufahamiana pamoja na kujenga mazingira
rafiki kwa wanafunzi wote pia kuwapa burudani pia kujijenga kisaikolojia kwani
michezo hujenga, kujumuika pamoja katika hafla hii itatuwezesha kuwa na
ushirikiano wa kutosha,” alisema.
MWISHO.