MSANII nyota wa muziki nchini Hussein Rashid maarufu kama Hussein Machozi amesema serikali ikisimamia kikamilifu sheria ya hati miliki, muziki wa Tanzania utafika mbali.
Machozi ambaye aliwika na kibao chake cha… na kupata tuzo ya mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki 2010 anasema, Tanzania inawasanii wenye uwezo wa kuimba vizuri na kutunga mashairi lakini wanashindwa kipiga hatua kutokana na kukosa hatimiliki.
“Muziki wa Tanzania bado haujapata nafasi ya kusikika katika nchi za wenzetu, wasnii wanauwezo mkubwa sana wa kuimba na kutunga mashairi, tatizo lililopo ni hatimiliki,”anasema.
Anasema, wasanii wengi wanandoto za kufika mbali kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye umaarufu ndani na nje ya Afrika lakini malengo yao yanakwamishwa na baadhi ya watu wanaojiita wasimamizi wa sanaa.
Akizungumzia albamu yake ya tatu anayotarajia kuikamilisha punde, Machozi anasema albamu hiyo itakuwa ya aina yake kutokana na kuwa na ladha tofauti tofauti na kwamba iko katika usimamizi wake mwenyewe.
“Albamu iko kwenye usimamizi wangu mwenyewe, na baadhi ya nyimba nimerekodia katika studio za Kenya, RK Production na MJ record kwa Tanzania,”anasema.
Machozi alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zimekamilika kuwa ni hellow Unanifaa na Mizimu na kwamba zitaanza kusikika kitaani muda mfupi.