BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, July 10, 2010

SUPERMODEL MILLEN ON THE COVER OF LADYBRILLE



HONGERA dada Happiness Magese (MILLEN), Kwa kushine katika tasnia nzima ya modeling kwa kupata nafasi ya ku cover katika from page kwenye magazine la LADYBRILLE lilitoka hivi June. mwanadad huyu aliyekuwa miss Tz miaka ya nyuma ametajwa kuwa mmoja wa atakayevaa taji la Queen of Africa In Fassion World ambaye kwa sasa anaishi nchini South Africa.

MKALI WA CINDELELLA ALIKIBA

Staa wa ngoma ya Cinderela aliyejiajiri kupitia game ya muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva, Ali Kiba anachana wazi kwamba dhuluma inayofaywa na baadhi ya mapromota wa kibongo ndiyo sababu kubwa inayomfanya kuzipa kisogo ‘shoo’ za Kibongo na ‘kulowea’kwenye steji za Ughaibuni.

ALI K

Mkali huyo ambaye bado anauza kupitia kazi zake za muziki hapa ‘Tizii’ na nchi za jirani, amedai kuwa alikumbwa na matukio mengi ya kudhulumiwa mkwanja wa shoo na mapromota uchwara wa Kibongo, kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza, akaamua kuziweka kando kwa muda shoo za kibongo

“Kuna watu fulani fulani hivi wanawaumiza sana wasanii, huku wakitangaza kuwasaidia na kuwainua, lakini ukweli ni kuwa jamaa ni watu wa dhuluma sana ndiyo maana mimi nakamua mbele kwa mbele ambako hakuna longolongo,” alitanabaisha staa huyo aliyewahi kukimbiza na ngoma yake, ‘Usiniseme.’

SARAH KAISI NA MUZIKI!.

Staa wa ngoma ya Shoga, Sara Kaisi a.k.a Shaa amefunguka na kuweka wazi kwamba, hivi sasa anaweza kuisaidia familia yake wakiwemo wazazi kwakuwa tayari ameshaanza kuchungulia mafanikio kupitia game ya muziki wa kizazi kipya.

SHAA

Akihojiwa na kituo kimoja cha Radio...hivi juzi kati,Shaa alisema sanaa ya muziki ambayo aliianza tangu 2004 hivi sasa imemfanya aishi vizuri huku akiisaidia familia yake kwa mambo mbalimbali ikiwemo kuleta misosi mezani.

“Huko nyuma wakati naanza muziki sikuwa na uwezo wowote, lakini sasa naweza kuwasaidia hata wazazi wangu,” alisema Shaa ambaye hivi sasa anafanya vizuri na kupitia kazi hiyo.

Hemedi Ajipanga Upya

HEMED (PHD)

thazealottz  ilibahatika kukutana na msanii aliyeng'aa sana kwenye shindano la tusker project fame, wengi wanamjua kwa jina la Hemedi aka Handsome Boy. Hemedi baada ya kumaliza mashindano ya tusker project fame alianza kujishughulisha na muziki bongo wa kizazi kipya. Msanii huyo aliachia single iliyomtambulisha iitwayo 'Ninachotaka' iliyofanya vizuri kwenye chati.
Hemedi aliweka wazi sababu yake kubwa ya kupotea kwenye game kwa muda mrefu,kuwa ni kwenda shule kumaliza elimu yake.Mfano mkubwa sana wa kuigwa na wasanii wenzake na Jamii kwa ujumla kwani anatambua umuhimu wa elimu.
Hemedi juzi kati alijiingiza kwenye mashindano ya kucheza 'serebuka' ambapo kwa kupitia twisti kali aliloonyesha,alifanikiwa kufanya vizuri sana na hata kukonga nyoyo za mashabiki japokuwa hakulitwaa taji hilo.
Hemedi ana machache tu ya kusema kufuatia ujio wake mpya, 'Kwa mafans wangu,ni kwa sababu yenu napika vitu studio na nina ahidi kitatoka kitu cha ukweli sana! Mkae tayari kujipangusaa, Raaah Raaah!'

Friday, July 9, 2010

Tha Zealot ndani ya "Mkesha wa Kazi"

Kutana tha Zealot katika kipindi cha "MKESHA WA KAZI" Bonge la show kuanzia mida ya saa 7 usiku mpaka saa 11 alfajiri,

 Tha Zealot

Kupitia show hii unapata nafasi ya ku request ngoma kali katika 9t kali kaa hii na kudedx it kwa memba watano yaaaaap watano bila Ubishi.

 Tha Zealot with Omar(jembe)

Pia mida ya saa kumi na moja ni kuamshana kwa njia ya simu katika segment ya amka na Sibuka fm mida ya saa 11 hadi saa 12.

Tukutane basi mida hiyo! 

GAMBE JINGINE katika show tight yaBAABKUBWA siku za ijumaa na jmosi na sunday kuanzia mida ya saa  4 mpaka ngoma 7 hivi pale kati nakupa milazo tuu non stop na info kibao za ma celebrity so kama vipi tuchekiane tyme hizo kupitia;

94.0 KWA PWANI NA DAR, 104.9 SHY TOWN NA 97.0 KWA MASWA PIA KATIKA SATELITE KUPITIA TBC1 KATIKA AUDIO 4 RIGHT pale katiiiiiiiiiiiiii mazeeeeeeee

 Tha Zealot with Omar(jembe)

Freequence zijazo kupitia Sibuka fm;

MWANZA 95.5, 
BUKOBA 92.6, 
KIGOMA 97.6, 
DODOMA 92.0, 
ARUSHA 104.6, 
MBEYA 97.6,
MTWARA 96.2

SIBUKA FM SAUTI YA JAMII YA AFRIKA YA MASHARIKI 

PAMOJA TUNAWEZESHA JAMII

TEEN EXTRA AWARD BADO LINI?!


Katika hali ya kusikitisha teen extra award zimezimika kama mshumaa kweye upepo. Teen extra award hizi ni tuzo zilizokuwa zimeandaliwa na timu nzima ya XXL kipindi maarufu kwa burudani Tanzania kinachorushwa na redio ya watu a.k.a Clouds FM, award hizi zilisikika na zilitangazwa kwa mbwembwe za kutosha kabisa mpaka kufikia hata kuipa
hofu timu uandaaji wa award za kili lakini cha kushangaza mbio zote zile zimepiga mweleka na kupotelea gizani na wala hatujui mchawi ni nani pande zile kwani hata wao wenyewe (waandaaji) hatuwasikii kabisa akilizungumzia jambo hili, mimi kama mdau wa sanaa nzima ya bongo nauliza niaje ni vipi?


Nilijiuliza kuwa Dozen, Fetty na Mchomvu kweli wameshindwa gemu au wamekula za uso!? Maana kiukweli hao ndio waliokuwa mstari wa mbele katika kuliandaa na kulifanikisha suala hili mpaka ilifika hatua ya kuzindua awrd zenyewe kwa mbwembwe kali mjini hapa kwa kufanya bonge la pati (sherehe) ya uzinduzi ambao walialika mpaka wasanii kwa kuwaimbisha pale CINE CLUB na kuwachezesha watu michezo kibao tu ya bichi, lakiniiiiii nikashangaa wameingia mitini wazeiya……..




Mnajua ni nini mazee!??! Kama vipi jipangeni upya mazee msikurupuke tu na kusema mnaanzisha kitu ambacho baadae mnakuja kuonekana kama ni mbio za sakafuni bana!

Kwa maana hata kwenye kumbukumbu zangu zinanipa na akili inanituma kwa konfince za kutosha kuwa inawezekana hata ile bash mlioinzisha na kuipa jina la INTER SCHOOL BUSH ambayo kwa mara yakwanza mliifanya mwezi wa saba mwaka jana (2009) pale kunduchi nalo pia mmengukia pua! Au sio?! Maana kwa kauli yenu wenyewe mlituambia kua tamasha lile litakuwa likifanyika kila kipindi cha mwisho wa likizo za wanafunzi likini pia na hilo chali?!

Kiukweli mkianza kitu mnajua ni jinsi gani mtakitasngaza maana katika suala la matangazo naweza kusema kuwa nawapa saluti lakini ikifika katika suala la uendelezaji hapo nipo ninakuwa na kigugumizi na wala sijui niwape aslimia ngapi kwa maana naona kama mnajaribu vile!?!

Haya maswali kibao yalisumbua sana hapa bongo5 lakini baada ya kujiuliza maswali yote hayo ilibidi bongo5 imtafute mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo ili kuzungumzia hili jambo. Bongo5 iliweza kumpata bwa Hamis Mandi a.k.a B12(B dozen) na alisema kilichowasibu mpaka tuzo hizo za teen extr kupiga mweleka.
Dozen alituweka wazi kuwa kweli wamekuwa kimya sana bila kueleza nini kitu gani kilitokea mpaka tuzo zikazimika kama mshumaa kwenye upepo. B12 mwenye manjonjo mengi wakati akiwa kwenye kipaza alisema “tuzo za Teen Extra zimezimika kwa sababu tulisimamishwa na basata kwa kile walichodai ni kuto zisajili, lakini sisi kama waandaji wa tuzo tuliona kama hakuna umuhimu wa kusajili hizi tuzo kwa sababu sisi tuzo zetu ni za muziki na masuala yote tunayofanya hapa XXL na ndio maana hata katika kategori zetu hatujaweka aina ya muziki zaidi ya bongo fleva, ila cha msingi ni kwamba tunasema tuzo hizo zipo na tutazitoa mara baada ya hili tamasha la fiesta kuisha”

Kuhusu suala la kuanzisha tuzo bila kuzisajili b12 alifafanua kwa kusema “huwa ni kawaida kwa kila tamasha kusajiliwa baada ya maandalizi yote kukamilika ili hata ukienda kusajili uwe na reference za kutosha na bajeti nzima ya tukio lenyewe”

Bwana dozen aliomba radhi kwa mashabiki kwa usumbufu wote uliojitokeza hapa kati na kuwa ahidi kuwa tuzo zipo na zitatolewa tu wala wasiwe na wasiwasi.

Beef ya Stiggo na Wakazi Yanukia



Watanzania Wawili waishio Nchini marekani Stiggo (pichani) ambaye ni producer wa S&S Records na ambaye aliwahi kuwa kwenye kundi la DIPLOMAT na Rapa machachali ambaye aliwahi kutoa mixtape yake hapa karibuni Wakazi ameandika kwenye facebook yake kuwa Stiggo ambaye anadai anamiliki Studio tatu nchini marekani ni uongo. Huu ni ujumbe ambao Wakazi ameandikakwenye facebook yake........


"S&S Records owner, Stiggo has been lying all along. he claims to own 3 studios in Brooklyn, Long Island and New Jersey. Apparently he be taking online recording studio pictures and claim its one of his. and does he really produce beats?! shouldn't he stick to rap, maa bad what rap....lol fake phony a**" ameandika Wakazi (pichani)
Moja ya studio anazodai kumiliki Stiggo ni hii:

Sunday, July 4, 2010

Prof J ndani ya USA



Professor Jay yuko ndani ya America tayari kwa kupiga Tour kali sana.
Show ya kwanza ni ndani ya Houston, ukumbi wa Safari,
leo usiku jumapili tarehe july 4, kusindikiza sikukuu ya uhuru wa marekani!!



Watanzania, wakenya, nyarwanda, uganda, congo, burundi, nk.
Wote mnaombwa mjitokeze kwa wingi kumpa support mtu wetu wenyewee!!