Baada ya kuambiwa hivyo jirani sijui aliogopa moyoni au ndo akaamua kumkomesha hasimu wake? Basi akapigia simu polisi, na wakaja kumkamata Foxy Brown, na kesi imeanza upyaaa. Foxy Brown hakuweza kupatikana ili acomment juu ya ishu hiyo.
Friday, July 23, 2010
Foxy Brown chini ya ulinzi baada kukwaruzana na Jirani yake
Baada ya kuambiwa hivyo jirani sijui aliogopa moyoni au ndo akaamua kumkomesha hasimu wake? Basi akapigia simu polisi, na wakaja kumkamata Foxy Brown, na kesi imeanza upyaaa. Foxy Brown hakuweza kupatikana ili acomment juu ya ishu hiyo.
Posted by thazealot at 7:30 PM 0 comments
MAISHA YA KIGANGSTER YAMPONZA DMX NA KUTOSWA NA MKE WAKE.
Tashera Simmons ametangaza kutengana na Rapa Earl Simmons a.k.a Dmx, na wakati huo huo anajiandaa kushoot kipindi cha Television/Reality show kinachohusu maisha halisi aliyopitia ndani ya ndoa yake na rapa Dmx hasa jinsi familia hiyo ilivyopigana na maisha wakati rapa huyo alipokuwa amebobea na madawa ya kulevya, pamoja na uhalifu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Tashera amesema katika Kipindi hicho pia ataelezea jinsi gani DMX alivyokuwa haijali familia yake. Mwanamama huyo anasema alianza mahusiano na Dmx Kuanzia akiwa na umri wa miaka 11 na alipofikisha miaka 18 ndipo alipoanza kuishi nae mpaka hivi karibuni alipotoka jela.
Tashera ameanzisha foundation inayoitwa WOMEN OF STRENGTH ambayo ni maalum kwa ajili ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, na unyanyasaji anaoupata mwanamke nyumbani. BADO Dmx hajajitokeza kuzungumzia ndoa yake, lakini mara ya mwisho alionekana wiki iliyopita, alipoungana na Kina Lil Kim katika kuperform ngoma ya kitambo sana inayoitwa Money Power Respect, jijini Newyork
Posted by thazealot at 7:18 PM 0 comments
Monday, July 19, 2010
LINNAH MSANII WA BONGO FLAVA ANAYETAMBA NA KIBAO CHAKE ATATAMANI MPATE KWA UNDANI SASA..
Mwenyewe anasema wimbo huo, halikuwa wazo lake..bali mashairi ya wimbo huo yalitoka kwa msanii mwenzake Amini ambaye naye pia ni uzao kutoka nyumba ya vipaji Tanzania 'THT'.
"Amini alikuwa akiuimba wimbo huu muda mwingi na tulipokuwa katika mazoezi nilipouimba alinikubali kwa kuwa nilikuwa naumudu vyema, hivyo akamweleza boss kwamba ni vema kama nikiimba mimi kwani ninafaa zaidi, ndipo nilipoingia studio na kuurekodi.
"Katika wimbo huu maudhui yaliyomo ndani yake ni kama yanafanana na kisa ambacho kilishawahi kunitokea mimi mwenyewe, lakini nilishangaa baada ya Amini kunipa yale mashairi nilihisi ameniona undani wangu.
Mrembo huyu aliyeanzia muziki kanisani tangu alipokuwa mdogo akiwa ni mtoto wa Mchungaji Petter Sanga wa kanisa la Glory of Christ anasema kuwa wazazi wake hawana tatizo na juu ya ulokole wao, wamekubaliana na mtoto wao ya kwamba atimize ndoto zake za kuwa mwanamuziki mkubwa wa kike.
"Wazazi wangu hawana tatizo na uimbaji wangu,kiukweli naweza kusema wamenipa baraka zao zote " anasema.
Binti huyu ambaye alisoma Msigani Sekondari ya Mbezi Louis iliyopo jijini Dar es Salaam anasema kwamba hivi sasa kuna wimbi kubwa sana la wasichana ambao wamejiingiza katika uasherati na utegemezi hali inayozidi kuwakandamiza katika dimbwi na umasikini na maradhi.
"Tusiwe tegemezi, wengi wetu wamekuwa wakijirahisisha kwa wanaume ili waweze kuwa na maisha mazuri, lakini mwisho wa yote ni kuzidi kujikandamiza katika maisha ya dhiki mbeleni" Anachokieleza mdada huyu ni kwamba wasichana wengi ni wavivu na wanapenda kujibweteka.
Posted by thazealot at 2:56 PM 0 comments
Mainda, Johari Wapikwa Pamoja
Vincent Kigosi almaarufu kama Ray ameondoa kile kinachosemekana kitaa kuwa yuko ndani ya bifu kubwa na waigizaji Ruth Suka maarufu kama Mainda na Blandina Chagula, Johari, baada ya kuwashirikisha kwenye filamu mpya iitwayo Bed Rest. Miezi iliyopita iliripotiwa kuwa muigizaji huyo ameingia kwenye bifu na waingizaji hao kwasababu zilizoelezwa kuwa ni za kimapenzi.
Akiongea na vyombo vya habari, Ray alieleza hakuna kitu kama hicho na anamshukuru Mungu kwa kumpa moyo wa uvumilivu na kutojali yanayosemwa.
‘Mimi ninaangalia kazi, na namshukuru Mungu ninaendelea kufanya vizuri. Hakuna tatizo kati yangu na Johari wala Mainda na ndio maana tunatoa filamu nyingine ya Bed Rest, iliyoandaliwa na RJ Company ambayo johari na mimi ni wakurungenzi’,alisema Ray.
Ray alisema safari hii ametoka na story itakayoacha simulizi kwa atakaye angalia.
‘Ina hadithi nzuri na tumewashirikisha nyota mahiri na chipukizi ambao wana uwezo mkubwa’ ,alisema Ray. Aliwataja washiriki wengine walioigiza kwenye filamu hiyo kuwa; Ndumbagwe,They naNurdin Mohamed chekibundi.
Posted by thazealot at 2:43 PM 0 comments
Bongo Star Search 2010 yanukia
Shindano la kumtafuta Bongo Star Search 2010 limetangwazwa rasmi kuanza na usaili kwa mwaka huu wa 2010 utaanza mkoani Arusha.
Tarehe 17-18th July itakua pale Impala Hotel Arusha.
Tarehe 24-25th July Itakua Dodoma Rock Hotel.
30-31st July Itakua Villa Park Resort Mwanza.
Tarehe 10-12th August itakua Coco Beach Dar Es Salaam.
Kama wewe unaona una kipaji na unataka kuwa star usisite kujitokeza siku na tarehe ambazo zimeandikwa hapo na ukajiandikisha.
Posted by thazealot at 2:39 PM 0 comments
Sunday, July 18, 2010
Mwisho Ndani ya Nyumba!!!
Shindano la Big Brother Africa 5 limeanza huko Mwisho Mwampamba akiwakilisha Tanzania ndani ya jumba la Big Brother. Mwisho aliwahi kushiriki katika shindano la kwanza kabisa la Big Brother mwaka 2003 na alijipatia umaarufu mkubwa alipoibuka mshindi wa pili nyuma ya kimwana Mzambia Cherise Makubale, aliyeibuka mshindi na kuzoa zawadi ya dola 100,000 (sawa na Sh. Milioni 130).
Baada ya Watanzania kuikosa kwa hatua chache tuzo hiyo ya BBA1, mashindano hayo ya runinga yalisimama kwa miaka minne na yaliyoporejea 2007, Richard Bezuidenhout, akafanya mambo. Akawa mshindi wa Big Brother Africa 2, akiwaacha washindani wake Tatiana, ambaye alikuwa mpenzi wake wa ndani ya jumba la BBA na Mnigeria Ofunneka, wakishika nafasi ya pili na ya tatu.
Mwaka uliofuata, Tanzania iliwakilishwa na Latoya Lyakurwa (2008) na Elizabeth Gupta (2009) ambao walitolewa mapema.
Wadau mnaonaje, Mwisho ataweza kujishindia hizo dola laki 2??
Posted by thazealot at 7:09 PM 0 comments