BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, October 15, 2011

Ditto na Linna washiriki kutoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wazee wenye ugonjwa wa ukoma.

WASANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Estelina Sanga maarufu kama Linna na Dotto Benard maarufu kama Ditto siku ya jumamosi waliungana na wadau wengine kutoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wazee wenye ulemavu wa ukoma ambao wanaishi katika kambi ya Nungwe maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili msanii wa muziki huyo wa bongo flava Ditto alisema kuwa wameamua kutumia fani ya muziki kama moja ya njia ya kujari na kutoa misaada kwa watu wasio jiweza.


“Kutoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wazee hawa ni jambo jema na sisi kama wasanii tunaitumia nafasi tuliyoipata kurudisha fadhila kwa watu wanaotupa msaada mkubwa katika kununua na kusikiliza kazi zetu,” alisema Ditto

Aliongeza kuwa wazee hawa pamoja na watanzania wengine ni kati ya kundi linalotoa mchango mkubwa kwa kuthamini kazi zao na wameamu kurudisha fadhila kwa wazee wasiojiweza ambao hali ya mazingira yao yalikuwa hayaridhishi.


Kwa upande wake Linna alisema kuwa wameona ni vyema kuungana na mradi wa Tanzania gives back (TGB) kutoa vifaa hivyo ili kupunguza adha ambazo zinaweza kuwapata wazee hao kutokana na mazingira yao kutokwa safi.

Alisema kuwa mradi huo ni wa kujitolea wenye lengo la kuhamasisha watu kujitolea katika shughuli mbali mbali kwa jamii zilizopo katika mazingira hatarishi.


“Sisi wasanii tunafaidika kupitia jamii ndio maana tumeona ni vyema kutumia kwa pamoja tunachokipata kwa kusaidia jamii inayotuzunguka,” aliongeza.

Alisema kuwa mbali na msaada huo waliotoa kwa wazee hao ambao serikali huwahudumia kutokana na ulemavu huo lakini pia waliweza kuwasihi wazee hao kutoa changamoto kwa vijana kujitolea na kujiajiri wenyewe ili kuachana na suala la kutegemea huduma kutoka serikalini.


Katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya milioni moja kutoka katika mradi wa TGB iliyofanyika katika kambi hiyo ya wazee pia ilihudhuliwa na mshindi wa tatu wa kinyang’anyiro cha Vodacom Miss Tanzania 2011 ambaye ni Alexia William.


 Kushoto ni Bw Edmond Lyatuu katikati ni Kemmy Mutahaba wakizungumza na  Bw Frank Munuo walipotembelea kambi ya wazee wenye ulemavu wa ukoma.
 Bw Edmond Lyatuu akimkabidhi Bw Frank munuo vifaa vya usafi wa mazingira katika kambi hiyo.
 Mr. Edmond Lyatuu akimkabidhi mwenyekiti wa wazee wenye ukoma vifaa vya usafi wa mazingira.
Wageni wa Tanzania Gives back wakielekea kumtembelea mmoja wa wazee ambaye anaishi katika kambi hiyo ambaye anauguza kidonda cha mguu.