Fainali za kumsaka mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro cha miss Tanzania 2010 imekamilika na mwanadada Genevieve Emmanuel aibuka mshindi wa kwanza kwa kunyakua taji hilo mwaka huu 2010/2011.
Mshindi wa pili ni Gloria Mwanga na mshindi wa tatu ni Consolata Lukosi ambaye pia ni Redds Ambassador mwaka huu 2010/2011.
Mshindi wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel.
Mshindi wa pili wa Vodacom Miss tanzania 2010, Gloria Mwanga katikati.
Mshindi wa tatu wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Consolata Lukosi.
Wadau wote wa blog hii ya www.thazealottz .blogspot.com na www.filamutanzania.blogspot.com pia.
Ninapenda kuwatakia Waislamu wote wa Tanzania Eid El Fitri njema. Muda huu wa kujitafakari unatukumbusha kuwa maadili ya uislamu wema, kujali wengine, kuhudumia jamii, ushirikiano na huruma ni amali ambazo sisi kama watanzania tunazithamini sana na ambazo kwa hakika zimechangia sana katika tamaduni nyingi duniani kote.
Eid Mubaraak kwa waislamu wote duniani.
Frank Aman Mawenya (tha Zealot).
Tuesday, September 7, 2010
Kwa sasa kupitia king'amuzi cha Startime tazama TV SIBUKA kwa movies kibao!
Na pata info kibao kuhusiana na vipindi vya TV SIBUKA kupitia
Na upate ratiba ya Movies zinazo oneshwa hapa kupitia
Lilian Andrew (kulia) mshindi wa tatu katika shindano la miss tabata mwaka huu akiwa na mshindi wa kwanza Consolata Lukosi (katikati) na (kushoto) mshindi wa pili cynthia shayo.
Baada ya mwanadada Lilian Andrew kutwaa taji la Miss TSJ kwa mwaka 2009 – 2010 mwezi April kwenye sherehe ya kuwakalibisha mwaka wa kwanza(Fresher’s Ball), kutoka chuo cha uandishi wa habari Time School of Journalism(TSJ), Hivi sasa kuna maandalizi kabambe kwa ajili ya kinyang’anyiro,muhula huu wa kumtafuta Mshindi mwingeine wa taji hilo la Miss TSJ ambalo Lilian alikuwa ni mshindi wa kwanza na Benadinna mwita alikuwa mshindi wa pili.Mwaka huu sherehe hizo za kuwakaribisha mwaka wa kwanza chuoni hapo zinatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi September mwaka huu katika viwanja vya Mbalamwezi Beach club na moja ya shamla shamla zitakazo kuwepo katika Bash hiyo ni pamoja na shindano hilo la kumtafuta mrithi wa mwanadada huyo.
Mshindi wa pili wa Miss TSJ Benadinna Mwita naye alishiriki Miss tabata
Blog hii ilipata nafasi ya kuzungumza na waandaaji wa Bash hiyo baadhi yao wakiwa ni viongozi wa serikali ya wanafunzi TISJOSO wamesema kuwa itakuwa ni moja ya Bash ambayo haijawahi kufanyika kwani kwa kupitia kinyang’anyiro hicho chuo kimejiandaa vizuri kwa kutafuta walembo wazuri wenye mvuto watakao kiwakilisha chuo hicho mwakani kwenye kinyang’anyiro cha miss Dar inter college,na pia kuna wadhamini baadhi wamejitokeza kwa ajili ya kutoa zawadi kwa washindi ambazo zitafahamika hivi karibuni.
Lilian Andrew akijibu maswali Miss tabata
Mwaka huu watu watakao shiriki katika shindano hilo ni Happiness Emmanuel, Juliana Victus, Sharifa,Aika,Irene na pia Judith Johnson na wengine wengi ambao bado majina yao hayakupatikana mapema.
Benadinna mwita akijibu maswali Miss tabata
Raisi wa serikali ya wanafunzi amewaomba wanafunzi kujitokeza katika bash hiyo na pia kutoa michango yao ili waweze kushiriki ambao ni tshs 15000/= kwa kila mmoja.
HARD PRICE COMING SOON
-
* Samahanini sana wadau wangu... Naombeni sana mnisamehe kwa kupotea kwa
kipindi kirefu, na yote haya yanatokana na majukumu ya hapa na pale. Ila
nisinge...
TSJ yang'ara mashindano ya Utangazaji 2013
-
*Frank Aman, *Mwananchi
*Dar es Salaam*. Chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism
(TSJ) kibeibuka kidedea kwa kupata alama za juu katika...
QUEEN SPEAR NI BALAA
-
*Hii ni Poster ya Queen Spear,iliyosheheni mastaa kibao..inatabiliwa kuwa
ni filamu itakayofanya vizuri sana katika soko la filamu Tanzania..Usikose
kunu...