BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, August 6, 2011

WAREMBO WA K'NDONI, TEMEKE, NA ILALA JANA WAANDAA FUTARI KWA WAANDISHI...

WAREMBO wa Redds Miss Ilala, Kinondoni na Temeke, mwishoni mwa wiki hii waliandaa futari kwa wahariri na wandishi kama sehemu ya shukrani kwa ushirikiano waliopata kihabari muda wote waliokua katika michuano ya kanda zao pamoja na kuwaaga wanahabari hao tayari kwa kuanza kambi ya taifa August 8.


. Picha ya pamoja ya warembo wa Miss Ilala, temeke na Kinondoni, wa kwanza kuria ni Redds Miss Temeke na wa pili kuria ni Redds Miss Ilala Salha Israel na wa tatu ni Redds Miss Kinondoni 2011 Stella Mbuge anayefuata ni Brand Manager wa Redds Victoria Kimaro, Mwanahabari na wanaogatia ni warembo walioshika nafasi ya pili nay a tatu katika kanda hizo..

Akizungumza katika hafla hiyo fupi. Mshindi wa Redds Miss Kinondoni Stella mbuge aliishikuru timu nzima ya waandishi wa habari za michezo na burudani kwa kumulika sanaa ya urembo na kuonyesha jamii kwamba ni sanaa yenye hadhi na nzuri tofauti na fikira za watu wengi.

“Uzoefu nilioupata katika mashindano haya nitautumia vizuri katika fainali ya MissTanzania na pia ningependa kuendea na fani hii ya urembo kwa kutoa elimu zaidi kwa warembo walioko vijijini na pia wapate hamasa ya kushiriki katika mashindano haya ili kutimiza ndoto zao,” alisema Stella.

warembo wa Miss Kinondoni, Ilala na Temeke wakibadilishana mawazo katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari na warembo hao.

Vile vile mrembo kutoka Redds Miss temeke Husna Twalib aliongeza kwa kusema kwamba moja kati ya sehemu ambazo alifurahia nikukutana na waandishi wa habari wa kike katika bonanza la michezo ambapo alipata nafasi ya kukutana na kubadilishana mawazo na wana habari mbalimbali, kitu ambacho kilimsaidia kupata uelewa wa kazi ya uandishi, na kitu ambacho angependa kukifanya katika siku za usoni.

Husna alisema kuwa ataitumia fani hii ya urembo vizuri katika kujenga mahusiano mazuri baina ya jamii na pia kuwasaidia watu ambao wana matatizo ya elimu hasa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi.

Baadhi ya warembo walioshiriki Mashindano hayo ya Urembo ya kanda tatu za Dar es Salaam wakichukua chakula (ftari) wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajli ya warembo hao pamoja na waaandishi wa habari iliyofanyika katika hotel ya city garden. (Picha na Frank Aman).

“Ningependa kusaidia watu ambao hawana elimu ama elimu yao iko chini kwa kuwashawishi wazazi wawaendeleze ama kutoa wito kwa taasisi na serikali kutilia mkazo wa elimu ambayo ndio nguzo ya maendeleo,” Husna aliongeza.

 
Mshindi wa Redds Miss Ilala Salha Israel alimalizia kwa kuwaaga waandishi hao na kuwasihi wazidi kuwa pamoja na warembo hao wakiingia kambi ya taifa ya miss Tanzania 2011, kwani wanaahidii kufanya vizuri katika ngazi ya taifa na kuahidi kuipaisha sanaa ya urembo.

Meneja wa kinywaji cha Redds, Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari ijumaa jioni jijini Dar wakati wa hfla fupi ya ftari iliyoandaliwa kwa ajili ya waandihsi wa habari na warembo wa kanda tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni. (Picha na Frank Aman).

Salha aliwasihi warembo ambao wameshiriki na hawakupata nafasi nzuri wasikate tamaa wajaribu kushiriki katika mashindano mbalimbali na watambue kuwa mashindano hayo si uzuri ama urembo wa mtu pekee bali pia nidhamu hasa unapokuwa kambini ndio kigezo kingine cha kukupa ushindi.

 

Sunday, July 31, 2011

Fiesta ilivyofana Dar

Ludacris on Stage

 Tip top Connection
 Mwana FA
 Crowd ya Fiesta
 Ludacris
 Audiences

 Farid Kubanda ama FId Q
Prof Jay