KUPITIA KING'AMUZI CHA STARTIMES NI SIBUKA TV KATIKA MAENENEO YA MWANZA , DAR , ARUSHA NA DODOMA UTAPATA NAFASI YA KUBURUDIKA NA KUHABARIKA NA KITUO HIKI BORA CHA TELEVISHENI KITAKACHOKUJIA HIVI KARIBUNI
Saturday, July 3, 2010
KUPITIA KING'AMUZI CHA STARTIMES NI SIBUKA TV KATIKA MAENENEO YA MWANZA , DAR , ARUSHA NA DODOMA UTAPATA NAFASI YA KUBURUDIKA NA KUHABARIKA NA KITUO HIKI BORA CHA TELEVISHENI KITAKACHOKUJIA HIVI KARIBUNI
Posted by thazealot at 6:25 PM 0 comments
104.9 fm, 97.0fm, 94.0 fm hii ni sibuka fm! PIA KUPITIA KING'MUZI COMING SOON NI SIBUKA TV
Kwa taarifa na burudani ni station hii tuu ndo yaweza kukupatia kile unachokihitaji katika nyaanja zote za burudani na habari.
Posted by thazealot at 6:13 PM 0 comments
SIKILIZA BAABKUBWA SAA 10:00 USIKU MPAKA SAA 01:00 USIKU KUPITIA SIBUKA FM
Posted by thazealot at 12:05 PM 0 comments
TUZO ZA BET SASA HIVI KATIKA BLACK ENTERTAINMENT TELEVISON
Tuzo za wasanii wa muziki wa Hiphop na RnB wenye asili ya kiafrika zilizofanyika tarehe 27.06.2010 zinaonyeshwa live sasa hivi katika television ya BET.
Nakusihi mdau wangu utazame kupitia katika vingamuzi vya STARTIMES ambavyo unapata nafasi ya kuona channel hiyo kwa hapa TZ.
Posted by thazealot at 11:41 AM 0 comments
Friday, July 2, 2010
SIKILIZA SIBUKA FM KWA PWANI, DAR, MASWA, NA SHINYANGA katika fm PIA SATELITE DUNIA NZIMA KUPITIA TBC 1 katika audio 4 right
VIPINDI:
SIKILIZA KUPITIA FM 94.0 DSM NA PWANI,97.0 MASWA, 104.9 SHINYANGA na KUPITIA SATELITE KWA TBC 1 TELEVISION.
Posted by thazealot at 7:42 PM 0 comments
TUZO ZA BET FUNIKA BOVU NIKKI MINAJ AUWAA
Best Female Hip Hop Artist: Nicki Minaj, Best New Artist: Nicki  Minaj, 
Best Male Hip Hop Artist: Drake, Best Group: Young Money

didy  na busta rhymes wakiperfom juu ya stage ya BET siku ya tarehe 27 yaahi  jana

Best  Male R&B Artist: Trey Songz

Best  Female R&B Artist: Alicia Keys, Best Collaboration pia ilienda kwa :  Jay-Z & Alicia Keys - Empire State of Mind

Chriss  brown alia stajini akiperfom nyimbo za michael jackson hasa alipokua  akiimba wimbo unaoitwa MAN IN A MIRROR
Posted by thazealot at 4:56 PM 0 comments
Lamar atoa ofa kwa wanadada!
Hapa nazungumza nikiwa kitaa cha Kariakoo...kunako studio za Fish  Crab...za bwana mdogo Lamar..ambaye anashikilia mkononi 
tuzo ya kili ya mtayarishaji bora wa muziki wa mwaka.
|  | 
ANASEMAJE MCHIZI HUYU
Ni kwamba mchizi anatoa offer bure ya kurekodi kwa underground wa kike popote pale walipo ndani ya bongo..ambao wanajihisi ama wanajiamini kuwa wana uwezo wa kurap au kuimba r&b,pop na mengineyo..na ambaye hayuko chini ya Record label yoyoye...kupeleka demo kwenye studio zake zilizopo eneo ya Jangwani karibu na klabu la Yanga ili ihakikiwe..na kama huna uwezo wa kutengeneza demo basi fika kwenye studio hizo na utapewa maelekezo ya kushiba uli ufanikishe azma yako! ewe mwanadada...time ndio hii..usipoteze muda.
Posted by thazealot at 4:16 PM 0 comments
Show za MBDOGGY zalalamikiwa Nchini UK
Msani MB-DOGG yupo nchini uingereza kwa ajili ya kupiga show kali nchini  humo, But baadhi ya wadau wamelalamika na kutatizwa na MBDOGGY kutumia  mtindo wa playback toka kwenye concert ambao Doggy katupia pale mji wa  milton keynes ..
PROMOTER WAPI LIVE BAND..NA NI KWANINI PLAYBACK ?????
Hapa sijajua kwamba msala nimtupie nani !!!!..tuanzie kwa huyu mletaji msani .promoter unamleta msani toka afrika alafu anaimba juu ya cd(playback) hapo lengo hasa la kumleta huyo msanii kwa wale mashabiki wake ni lipi...? kama anaimba na cd..mie nilikuwa nafikiria kuwa ma promoter jaribuni kuwa sistizia wasani ambao mna wapeni mashavu ya kwenda nje kutangaza sanaa yao..waiimbe kupitia live band sio mambo ya play back cd..hapo tutakuwa tunainua na kukuza vipaji na vile vile kunenepesha mifuko ya wasani hao..coz ..naona wasani wanao imba live music mashabiki wao wana furahi na vile vile kuwaleta wasani kama wale ni gharama coz wanatoa burudani halisi sio cd play back..lakini mkaka DOGGY hongera but step up the Game to live band music kaka ..hicho ndio kitu ambacho dunia inataka kutokwa kwa wasani halisi sio wababaishaji..
Posted by thazealot at 4:12 PM 0 comments
Thursday, July 1, 2010
Mixtape ya Antivirus inatetea muziki wa bongo flava? Sugu Azungumzia kukamatwa kwake:
Nyimbo ya I Wanna Kill Ru.., unaopatikana kwenye mixtape hiyo  umepelekea Sugu kuitwa na kuhojiwa na polisi. Pamoja na mistari ya  nyimbo hiyo kuwa mikali kidogo, lakini je, ni kweli kuwa Sugu anataka  kuua au ni utundu tu wa mashairi?
Mixtape hii imeibua hoja  kadhaa, moja ikiwa ya uhusiano kati ya redio na wasanii,     pamoja na nafasi ya redio katika kukuza sanaa nahata nafasi ya redio  kuuwa sanaa. Neno bongo flava lilizaliwa redioni, na redioni huko huko  ndipo bongo flava ilipolelewa na kukuwa mpaka hapa ilipofikia. Lakini  je, redio zimefanya kazi ya kutosha kukuza ubunifu katika sanaa hii ya  bongo flava? Kwani, swala la ma-Dj kuwa mameneja wa wasanii linapigiwa  kelele kila siku, kwani ma-dj hao mamaeneja wanashukiwa kuwapendelea  wasanii wao. Kama hii ni kweli, upendeleo huo ni ufa, tena ni ufa  unaoweza kuhatarisha maendeleo ya sanaa hii inayoajiri vijana wengi.
Pamoja  na yote, mashairi ya Sugu na wenzake katika mixtape hii yanaweza  kuangaliwa katika pande mbili. Pande ya kwanza, ni kuwamashairi yao  yanachochea chuki na hata kuleta fujo. Pande ya pili, ni kuwa mashairi  yao yanaongea ukweli mtupu, na lugha kali waliyotumia ni kutokana na  kuchoshwa na unyonyaji katika sanaa ya bongo flava. Inawezekana pia Sugu  ameamua kujitoa muhanga na kutuonesha roho ya udhubutu, kwani  Watanzania tuna sifa ya kukubali yaishe. Sasa basi, kama mashairi ya  mixtape hii yataleta fujo, Sugu na wenzake watakuwa na kesi ya kujibu.  Lakini kama tunakubaliana kuwa mabadiliko “changes” huja mara nyingi  kutokana na mapambano ya aina fulani, basi Sugu ndio anatuonesha njia,  kama Bob Marley alivyoimba Get Up Stand Up.
Swali, je Mixtape ya  Antivirus inatetea muziki wa bongo flava dhidi ya wachache  wanaouyumbisha au inataka kuchochea fujo zinazotokana na chuki  kibinafsi? Sasa soma tamko rasmi alilotoa Sugu kwa vyombo vya habari juu  ya kasheshe zilizomkumba siku mbili hizi tangia Mixtape ifike mtaani.
**********************************************************************************
Barua  Ya sugu
napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu  wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA  na watanzania kwa ujumla tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa  kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia  kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo  kwenye album iitwayo “Anti Virus”.
Walinikamata saa 5 asubuhi  nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya  kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake  nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.
Wameniachia  kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na  kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi  siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini  kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho  ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.
Katika mahojiano nao  yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani;  maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio  cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba  mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.
Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba  nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno  niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote.  Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za  kifasihi.
Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati  zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya  wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua  dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.
Ni vyema mashabaki wangu,  wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi  mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba  pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.
Katika wimbo huo nimeghani  kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na  wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai;  hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na  hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya  kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.
Aidha  nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya  Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya  ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya  Kinondoni.
Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa  jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi  na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa  wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza  nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai  badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo  yana sura ya madai yasiyo na uzito wowote.
Posted by thazealot at 6:29 PM 0 comments
Fiesta 2010 kuanzia Mkoani Morogoro
MARLAW
Tamasha la Fiesta 2010 linakaribia kuanza,na kama ujuavyo tamasha hilo husheheni mambo kibao kwa wapenzi/washabiki wao.safari hii kwa mara ya kwanza tena linagonga hodi ndani ya mji kasoro bahari,Morogoro.Wakazi wa Morogoro Fiesta hiyo 2010 inawajia mkoani mwenu ikiwa na kauli mbiu yake JIPANGUSE Rrrrrrrhhhhhhaaaaa..! Huku Mdhamini mkuu wa tamasha hio ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd.
MWANA FA & AY
Orodha ya wasaniii utakao Jipanguse nao ndio kama hao hapo juu,si hao tu na kuna wegineo kadhaa wa kadhaa akiwemo Mwana Fa,Amini na Linah kutoka THT.Kutakuwepo na michezo mbalimbali,Fiesta Jipanguse rrrhhhhhaaaaa 2010 itafanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri,July 7 kwa kiingilio cha sh 2000 kwa kila mmoja.Kama vile haitoshi July 9 tamasaha hilo litahamia mjini Arusha na kufanyika ndani ya Matongee .
Posted by thazealot at 6:15 PM 0 comments





















 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 


 
 Posts
Posts
 
 
