Hapa nazungumza nikiwa kitaa cha Kariakoo...kunako studio za Fish Crab...za bwana mdogo Lamar..ambaye anashikilia mkononi
tuzo ya kili ya mtayarishaji bora wa muziki wa mwaka.
ANASEMAJE MCHIZI HUYU
Ni kwamba mchizi anatoa offer bure ya kurekodi kwa underground wa kike popote pale walipo ndani ya bongo..ambao wanajihisi ama wanajiamini kuwa wana uwezo wa kurap au kuimba r&b,pop na mengineyo..na ambaye hayuko chini ya Record label yoyoye...kupeleka demo kwenye studio zake zilizopo eneo ya Jangwani karibu na klabu la Yanga ili ihakikiwe..na kama huna uwezo wa kutengeneza demo basi fika kwenye studio hizo na utapewa maelekezo ya kushiba uli ufanikishe azma yako! ewe mwanadada...time ndio hii..usipoteze muda.
0 comments:
Post a Comment