BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, August 28, 2010

KUPITIA JUKWAA LA FILAMU LEO PATA HABARI HIZI

Saturday, August 28, 2010


Nollywood DIVA, OGE OKOYE azungumzia kuhusiana na familia.



 Oge Okoye-Duru


MSANII maarufu wa kike, Oge Okoye ambaye ameolewa na mfanya biashara maarufu wa kimataifa, Stanley Duru amejifungua. Msanii huyo nyota, Oge alijifungua mototo katika hospitali Queen Elizabeth,London. Aliondoka nchini humo akiwa amebakiza mwezi mmoja ajifungue kuelekea London na alirejea akiwa na‘Bigie Bigie Bouncing Baby’. Alipata nafasi ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na moja ya chanzo cha habari Bi ALONGE MICHAEL na akazungumzia na furaha aliyonayo,baada ya kuwa mama. Mazungumzo yalikuwa hivi
KWA NINI UMECHAGUA KWENDA LONDON KWA AJILI YA KUJIFUNGUA?
Nimeona itakuwa rahisi sana London Uingereza kuliko nchi nyingine. Lakini usisau kuwa nilizaliwa hapa pia.

UNAJISIKIAJE SASA UMEBARIKIWA KUPATA WATOTO WAWILI WA KIUME NA WA KIKE?
Nina furaha sana na nina mshukuru mwenyezi Mungu kwa kunifanya kuwa mwanamke niliyekamiliaka. Unajua , furaha ya kila mwanamke ni kuwa na motto wa kike na wa kiume. ingawa, wazazi wengine wanapendelea jinsia moja, katika suala letu, tulikuwa na mtotot wa kwanza wa kiume na sasa wa kike, hatutarajii tena kujaaliwa kuwa na mwingine. Najisia Furaha.

JINSI GANI UTAWEZA KUWALEA WATOTO HAWA UKIZINGATIA NA MAZINGIRA HASA KATIKA FANI YAKO KWA KUWA WEWE NI MUIGIZAJI?
Hiyo sio issue sana. Nilipopata mototo wa kwanza, nilipata msaada kutoka kwa mama yangu na kwa wasaidizi wangu pia. Sikuruhusu movie kuharibu uhusiano wangu na mtoto. Nilikuwa najitahidi kuja mapema kuhakikisha motto yuko salama, ingawa, mama yangu alikuwa karibu kumwangalia  mpaka anakua.

HIVYO NI LINI HASA UNATARAJIA KURUDI KATIKA LUNINGA?
ki ukweli siwezi kususbili kurudi. Kabla sijaondoka kwenda London kwenye safari yangu, nilikuwa tayari nina kama script 9 katika shelve yangu, nilitegemea kwamba ningeweza kufanya movie kabla sijaondoka lakini haikuwa rahisi kwangu. Hata hivyo baadhi ya movie zimesogezwa na maproduzya wamenisisitiza  nirudi kuchukua nafasi yangu. Hivyo, sasa nimeshapona vizuri, sina jinsi zidi ya kurudi location na kumalizia movie hizo. Unajua, movie kwangu ni zaidi ya pesa, ni kitu napenda lazima nikikamilishe.
WATOTO WANGAPI UNATARAJIA KUWA NAO ZAIDI?
Idadi ya watoto tunayo hitaji inategemea na Mungu atatupatia wangapi. Kama akisema kumi 10, mimi ni nani nikatae?. Mungu ndiye ana maamuzi juu ya hayo.

STANLEY ANAZUNGUMZIAJE KUHUSIANA NA MAENDELEO HAYA?
Wee unahisi atajihisije? Furaha kabisa!anafuraha sana na haishi kushukuru mungu kwa kutufikisha mbali..

ALIKUWEPO KARIBU NAWE ULIPOKUWA LABOUR?
Hayo ni personal kwangu. Mashabiki wangu hawapaswi kujua kuhusu hilo, ukweli unabaki kuwa ukweli, alikuwa na mimi muda wote.

UTWABATIZA API WATOTO WAKO?
Hakuna kitu bora kama nyumbani, tunakuja Nigeria kwa ajili ya ubatizo wa wanangu. Muda ukifika tutawaalika ndugu,jamaa na marafiki kujumuika pamoja kusherekea.

Francis Duru na Wasanii wengine wa Naija wakanusha kupokea Naila 300, 000/=

 Francis Duru

MUIGIZAJI kutoka Nollywood, Francis Duru, amekanusha kupokea pesa kutoka kwa Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kama takrima kwa ajili ya kampeni yauchaguzi mkuu wa awamu ya nne utakao fanyika mwaka 2011.

Imelezwa kuwa, Duru, na wasanii wengine nyota 50 kutoka Nollywood, walipokea Naila 300, 000/= kila mmoja kwa ajili ya kampeni ya Rais Jonathan, baadhi ya wasanii nyota wamekanusha habari hiyo. Wamesema kuwa wameungana kwenye kampeni hiyo kwa sababu wanaamini Jonathan ni kiongozi mwenye malengo thabiti na yenye mabadiliko.

Msanii huyo nyota amesema: “Inafurahisha kuona baadhi ya wenzangu wakishikia kidedea suala hili. Ni ajabu sana kuwa watu wameacha shughuli zao za kila siku na muda wao na kufanya hivyo kwa kuwa tuu wanaamini. Hawalipwi chochcote kwa kazi hiyo. Na ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kwa mapenzi yao tuu, kumsapoti na kumwamini. Na kwa mimi, Jonathan ndiye mwanaume, nimemuona, nimekutana nae, nimeona kazi yake na ninajua anastahili kushika wadhfa huo.”

Mpango huo, ambao unaratibiwa na msanii Richard Ossai, ukisapotiwa na Mheshimiwa Ned Nwoko na kudhaminiwa na Sea Petroleum na Gas boss, Stella Odua, wameandaliwa kuhakikisha ushindi wa Jonathan katika ngazi ya urais.

Wakati huo huo wasanii 31 kutoka naija wamekamilisha kurekodi wimbo maarum kwa ajili hiyo utakaojulikana kama Goodluck 2011, uliotayarishwa na produzya aliyeshinda tuzo, Cobhams Asuquo, Pia wasanii wengine 20 nao pia wamekamilisha kurekodi wimbo mwingine wenye mahadhi hayo utakao julikana kama, Goodluck 2011.

Wasanii baadhi walioshiriki ni pamoja na mshindi wa tuzo za nyimbo za injili Sammie Okposo, African Chyna, Daddy Showkey, Zaaki Adzee na Tosin Martins .

Kundi la Kampeni yaGoodluck liko chini ya Barrister Gullac, ambaye anajitahidi kwa hali na mali kila wakati kuhakikisha linafanikiwa kupitia kwa wasanii hao.

Wednesday, August 25, 2010



Kampuni ya Clouds Media Group kupitia Clouds TV jana jioni imefanya uzinduzi wa kipindi bora cha TAKE ONE chini ya mtangazaji Zamaradi mketema mwana dada mahiri katika mambo ya uchambuzi wa habari za wasanii wa filamu na filamu hapa nchini, kitakachohusu tasnia ya filamu hapa nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa vipindi vingine vitakavyokuwepo katika Clouds TV na uzinduzi huo uli ruka live kupitia channel hiyo, sherehe hiyo iliwaalika wadau na wasanii mbalimbali wa filamu  hapa nchini



Zamaradi Mketema na Ephraim Kibonde.
Kupitia kipindi hiki tasnia ya filamu hapa nchini itaweza kupanuka kwani kumekuwa na uchache wa vipindi hivi vinavyojihusisha na tasnia hii ambapo kimojawapo ni kipindi cha TV kinachorusha na televisheni ya EATV kwa hapa Tanzania chini ya mwanadada Joyce Kilya.



Zamaradi mketema

Tuesday, August 24, 2010



Msanii nyota wa filamu hapa nchini Daudi Michael amekamilisha utayarishaji wa filamu zake na hivi sasa zimeanza kuingia sokoni moja kati ya filamu ambazo zimeingia sokoni ni Fake pregnant na moja ambayo haaijatoka kwa sasa Aunt suzzy.ambazo ametayarisha hivi karibuni.
Amesema kuwa filamu hizo ni bomba na zinazungumzia maisha halisi ya kitanzania.

 DVD cover ya filamu ya Fake Pregnant part one

DVD cover ya filamu ya Fake Pregnant part two.
Pia amesema kuwa wasanii nyota walioshiliki katika filamu hizo ni kama Esther,sarah sudi, sudi,santana na wengine nyota kibao na wasanii vichwa wachanga.

DVD cover ya filamu ya Aunt Suzzy part one.
DVD cover ya filamu ya Aunt Suzzy part two.
Zaidi msanii huyu wa filamu hapa nchini ameshatoa filamu kadha wa kadha kutoka katika kampuni yake ya D production kama vile Where is love, Upside Down, Remember na nyingine kibao.na amewahi kushiriki katika movies nyingine kama money desire,kisisina and many more.
Hivyo amewaomba watanzania wamuunge mkono katika kazi yake kwa kununua nakala halisi ili tasnia nzima ya filamu iweze kusonga mbele na ameahidi utakapo nunua filamu hizi hutajutia maamuzi yako. 
Wabongo tumuunge mkono mbongoo mwenzetu tuachane na mambo ya kale ya tamthilia za kiphillipino eti jamani.........!!

0 comments: