BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, September 12, 2010

Mambo manne ya kuzingatia Kama unataka kuacha/kupunguza pombe!



Pombe ni burudani, huondoa uchovu na kuchangamsha mwili, lakini wakati mwingine pombe ikimzidi mtu huweza kumharibia hata mipango mbalimbali ya maisha yake. Hapo sasa ndipo shauku ya mtu kutaka kuacha pombe inakuja.

Hata hivyo, pamoja na shauku hiyo ya kuacha pombe, wengi hushindwa kutokana na mwili wake kuwa tayari umeshazoea pombe. Hapa nitakupa njia za kitaalamu kabisa ambazo ikiwa utazitumia kwa umakini, inaweza kuwa rahisi sana kwako wewe mlevi kupunguza kama siyo kuacha kabisa kunywa pombe.

Sasa soma mtiririko ufuatao.

KIMBIA KAMPANI ZA POMBE
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo unatakiwa kuifanya wewe ambaye una nia ya kupunguza au kuacha kabisa kunywa pombe. Achana na marafiki zako walevi, usipende kufanya vikao katika baa au kumbi za starehe.

TAFUTA VITU VYA KUFANYA
Wahi kufika nyumbani, na tafuta vitu vingine vya kufanya kama kusoma magazeti, kuangalia filamu na mengine mengi ya kupendeza. Ni rahisi tu kufanya hivyo. Kwanza uanweza ukabadilisha ratiba yako ya kazini. Jiongezee ubize kwa kadri uwezavyo, ili utakavyotoka kazini uwe mchovu, unayewaza maji ya kuoga na kupumzika huku ukipata burudani nyingine kama nilivyoeleza hapo juu.

BADILI VINYWAJI
Kwakweli ni vigumu sana kuacha pombe, lakini kama una nia ni rahisi pia. Pindi uhisipo hamu ya kunywa pombe, tumia muda huo kunywa chai, kahawa, juisi au maziwa. Kwa kawaida, baada ya kunywa vinywaji vya baridi au moto vyenye sukari, hukata au kupunguza hamu ya kunywa pombe.

AMUA KWA DHATI
Pamoja na yote hayo niliyoyafafanua hapo juu, ni jukumu lako wewe na moyo wako kuamua kwa dhati kabisa kwamba “SASA HUTAKI TENA KUNYWA POMBE! Ikiwa utakuwa na imani hii moyoni mwako, ni rahisi sana kuacha pombe.


0 comments: