BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, October 9, 2010

Historia fupi ya consolata Lukosi na ndoto zake za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa.


Jina lake halisi ni Consolata Lukosi,Ana umri wa miaka  20,anakotoka ni manispaa ya Ilala,Kabila lake Mhehe Consolata ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia ya Bwana na Bi. Lukosi. alizaliwa mpanda mkoa wa Rukwa na baadaye kuhamia Mbeya na kujiunga shule ya msingi ya Isanga. Elimu ya sekondari ameisoma Mbeya Secondary School, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Baada ya hapo alihamia Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Jitegemee, aliposoma kidato cha tano na cha sita.


Consolata anasema fani ya urembo ni  fani ambayo alikuwa anaipenda sana tangu utotoni na pia ilikuwa ni kati ya malengo aliyodhamiria kufanikisha. Alianza kufanya mambo ya urembo kupitia kitongoji cha Tabata aliposhiriki na kushinda Miss Tabata 2010. Baada ya hapo alifanikiwa kuingia kambi ya Miss Ilala kuwania taji hilo, ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu .
  
Consolata angependa kuwa mfanyabiashara wa kimataifa aliye na kampuni yake binafsi na vilevile kuendelea kujihusisha na fani ya urembo hasa kupitia, uwanamitindo. Hivi punde atajiunga na chuo cha Learn It ambapo atachukua kozi ya biashara itakayomuwezesha kufanikisha lengo lake la kuwa na kampuni na kuwa mfanya biashara bora.
  
Akizungumzia kazi anazo fanya na kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji cha REDDS Consolata ameanza kwa kusema ana furaha kubwa sana kuwa na bahati ya kuwa balozi wa Kinywaji cha Redds kwa mwaka wa 2010. "Ninapokea kazi nzuri ya yenye heshima walizofanya wenzangu Victoria, Jokate na Natalia. Walikuwa ni mabalozi wazuri sana na kupitia ushauri na uongozi wao natarajia kufanya kazi itakayoleta mabadiliko kwangu na kwa jamii yangu na pia kwa Redds na kampuni ya Tbl" asema Consolata.
               
Anatazamia kufanya kazi kwa ukaribu sana na jamii hasa kupitia shughuli za kampuni mama ya kinywaji cha Redds, ambayo inatarajia kuanzisha miradi mbalimbali ya maji nchini na vilevile kwa kuwa kinywaji cha Redds kinajihusisha moja kwa moja na kuimarisha sekta ya ubunifu na mitindo anasema atakuwa mstari wa mbele katika shughuli zitakazoihusiana na uimarishaji huu. Vilevile anatarajia pia binafsi kuisaidia jamii yake kwa kupigania haki za wanawake na watoto pamoja na kuielimisha jamii kuhusu kujiepusha na majanga kama Ukimwi na namna ya kujiepusha nayo.


Consolata anachowambia ma miss   ni kuwa angependa wajue kuwa yahitaji sana moyo kuwa katika fani hii hivyo wasikate tama na kwa wale ambao hawakufanikiwa kufikia ngazi ya taifa wasisite kujaribu tena na pia waendelee kusoma na kujiendeleza katika shughuli za kuwaletea maendeleo wao na jamii inayowazunguka..
kwa sasa Consolata anaishi YomboVituka na Dada yake.



0 comments: