Peter Msechu
HII ni season ya nne tangu shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la TUSKER PROJECT FAME lianzishwe na kampuni ya bia ya EAST AFRICA BREWELIES LIMITED kupitia kinywaji chake cha Tusker, tumeweza kuona baadhi ya watanzania wakijitahidi kushiriki katika ushindani huo kwa hali na mali ili kuweza kufanikisha kuchukua ushindi huo lakini kwa bahati mbaya nchi yetu haijawahi kupata ushindi kutoka kwa hao wawakilishi wetu walioenda kushiriki katika TUSKER PROJECT FAME.
Kuna wawakilishi tofauti tofauti walioshiriki kuweza kuiwakilisha TZ mmoja wapo ni hemed, Alex, na wengine wengi.Lakini katika season hii ya nne tuliwakilishwa na Aneth pamoja na Leah Mou, Cynthia na Peter msechu na waliobahatika kufika nafasi nzuri katika shindano hili ni Leah,Aneth ambao walitoka hivi karibuni kwa kukosa kura za kutosheleza. Mpaka hivi sasa Tanzania bado inawakilishwa na Mwana kaka PETER MSECHU ambaye kwa wiki iliyopita aliingia katika probation na kwa sasa anaelekea kutoka endapo waTanzania hatutashirikiana kumpigia kura ili aendelee kuwepo.
Leah
Aneth
Ni ombi langu kuwa ili muwakirishi wetu aendelee kubaki katika mashindano ni vyema tumpie kura ili azidi kuwepo na kufanya vizuri na mwisho wa siku arudi na ushindi nyumbani ili kufuta historia iliyopo katika mashindano hayo kwa TZ.
Jinsi ya kumpigia kura PETER MSECHU aendelee kuiwakilisha TANZANIA andika neno TUSKER 9 tuma kwenda 15522 kupitia kura yako utakuwa umeweza kumpa nafasi PETER MSECHU kubaki katika TPF 4 na kuzidi kufanya vizuri na kurudi na ushindi.
WATANZANIA TUSHIRIKI KUPIGA KURA NA PIA TUOMBE MUNGU MUWAKIRISHI WA TANZANIA PETER MSECHU AFANYE VIZURI….
0 comments:
Post a Comment