MSANII wa vichekesho nchini Hillary Daudi (Zembwela) hivi sasa sauti yake inasikika ikirindima kupitia Redio East Afrika katika kipindi cha Super Mix akiwa na mtangazaji mahiri wa kipindi hicho Mussa Hussein, ushirikiano wa watangazaji hawa umeongeza burudani kama si ladha katika kipindi hiki cha Super Mix.
Zembwela alivuma sana katika vichekesho kipindi kirefu hasa wakati ule akiwa na marehemu Max walikuwa ni burudani ya kutosha wakati ule walikuwa wakitumiwa na kundi la kaole Sanaa Group kupewa sehemu fulani kwa ajili ya vichekesho lakini muongozaji wa kundi hili Chriss Mhenga kwa wakati ule baada ya kubaini vipaji vya jamaa aliamua kuwatenga na wasanii wa igizo na kupewa kipindi chao.
Hapa ndipo ilipozaliwa Mizengwe na kuteka hisia za watazamaji hata baada ya kufariki Marehemu Max Zembwela aliliongoza vema kundi lile na kuendelea kuwashika watazamaji katika masuala ya uchekeshaji akishirikiana na msanii mwezake Mkwere na baadae alipumzika na sasa wapenzi wake wanaendelea kupata burudani ya sauti yake kupitia Redio ya East Afrika.
“AFRICAN BEAUTY” IS JUST ANOTHER ONE FROM DIAMOND PLATNUMZ & OMARION WHICH
MIGHT BE THE JAM OF THE CONTINENT
-
The Tanzania Recording Artist Diamond Platnumz released “African
Beauty” off his just premiered album “A Boy From Tandale”. The album
features Top Artist...
6 years ago
0 comments:
Post a Comment