BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, December 5, 2010

DAVIS NTARE AJISHINDIA MIL.5 KSHS TUSKER PROJECT FAME 4.

Mshiriki DAVIS HILLARY NTARE aliyeshiriki mashindano ya kuibua vipaji vya uimbaji hapa Afrika ya mashariki na kati la TUSKER PROJECT FAME, ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambacho kinahusisha nchi sita kutoka Afrika Mashariki. Davis amejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 5 za kenya. 

Hii ni mara ya pili kwa nchi ya Uganda kunyakua ushindi huo, kwa mara ya kwanza katika Tusker Project Fame season 2 ushindi ulichukuliwa na Esther Nabaasa, na PTF3 ushindi ulikwenda kwa Alpha kutoka nchini Rwanda ambaye pia aliibuka tena mshindi katika tuzo za PAM akiwa kama PAM best artiste from Rwanda.

TANZANIA ikiwa kama washiriki katika shindano hilo imeweza kushika nafasi ya pili ikiwakilishwa na PETER MSECHU, nafasi ya tatu imeshikwa na STEVEN kutoka Kenya na nafasi ya nne ikiwa imeshikwa na AMILEENa kutoka Kenya pia.
Nampongeza sana Devis kwa ushindi huo, pia Msechu kwa kuweza kufika nafasi hiyo kubwa ambayo Tanzania hatujawahi ifika kwa mashindano hayo, pia nampongeza kwa kuweza kuiwakilisha Tanzania ipasavyo, bila kuwasau washiriki wengine kutoka Tanzania, Leah Moud, Aneth,na Cynthia ki ukweli wamejitahidi sana.

Changamoto kwa watanzania wenzangu jamani tushiriki kikamilifu katika kuwasappoti wenzetu wanapokuwa katika mashindano hayo ili na sisi siku moja tuweze kunyakua ushindi huo. Tujitolee kuwapigia kura washiriki kwa kila tuwezavyo kwani kilichomwangusha Msechu ni kura na sio suala la uimbaji..

0 comments: