BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, September 5, 2010

MISS TSJ 2010 – 2011 KUFANYIKA TAREHE 18/09/2010 MBALAMWEZI BEACH



 Lilian Andrew (kulia) mshindi wa tatu katika shindano la miss tabata mwaka huu akiwa na mshindi wa kwanza Consolata Lukosi (katikati) na (kushoto) mshindi wa pili cynthia shayo.

Baada ya mwanadada Lilian Andrew kutwaa taji la Miss TSJ kwa mwaka 2009 – 2010 mwezi April kwenye sherehe ya kuwakalibisha mwaka wa kwanza(Fresher’s Ball), kutoka chuo cha uandishi wa habari Time School of Journalism(TSJ), Hivi sasa kuna maandalizi kabambe kwa ajili ya kinyang’anyiro,muhula huu wa kumtafuta Mshindi mwingeine wa taji hilo la Miss TSJ ambalo Lilian alikuwa ni mshindi wa kwanza na Benadinna mwita alikuwa mshindi wa pili.Mwaka huu sherehe hizo za kuwakaribisha mwaka wa kwanza chuoni hapo zinatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi September mwaka huu katika viwanja vya Mbalamwezi Beach club na moja ya shamla shamla zitakazo kuwepo katika Bash hiyo ni pamoja na shindano hilo la kumtafuta mrithi wa mwanadada huyo.
 Mshindi wa pili wa Miss TSJ Benadinna Mwita naye alishiriki Miss tabata



Blog hii ilipata nafasi ya kuzungumza na waandaaji wa Bash hiyo baadhi yao wakiwa ni viongozi wa serikali ya wanafunzi TISJOSO wamesema kuwa itakuwa ni moja ya Bash ambayo haijawahi kufanyika kwani kwa kupitia kinyang’anyiro hicho chuo kimejiandaa vizuri kwa kutafuta walembo wazuri wenye mvuto watakao kiwakilisha chuo hicho mwakani kwenye kinyang’anyiro cha miss Dar inter college,na pia kuna wadhamini baadhi wamejitokeza kwa ajili ya kutoa zawadi kwa washindi ambazo zitafahamika hivi  karibuni.
 Lilian Andrew akijibu maswali Miss tabata



Mwaka huu watu watakao shiriki katika shindano hilo ni Happiness Emmanuel, Juliana Victus, Sharifa,Aika,Irene na pia Judith Johnson na wengine wengi ambao bado majina yao hayakupatikana mapema.
 Benadinna mwita akijibu maswali Miss tabata



Raisi wa serikali ya wanafunzi amewaomba wanafunzi kujitokeza katika bash hiyo na pia kutoa michango yao ili waweze kushiriki ambao ni tshs 15000/= kwa kila mmoja.

0 comments: