BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, August 7, 2011

CHUO CHA TSJ CHANG'ARA KWENYE MASHINDANO YA UTANGAZAJI..


Mkuu wa Chuo Cha TSJ Bi Setumbi

CHUO cha Uandishi wa habari cha Time School of Journalism (TSJ) kieibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kitaaluma yaliyoshirikisha vyuo vinne vya taaluma hiyo jijini Dar es Salaam.

Vyuo ambavyo vilishiriki katika mashindano hayo ni Time School of Journalism (TSJ), Royal College of Tenzania (RCT), Dar es Salaam School of Journalism (DSJ), na Dar es Salaam City College (DASICO).

Katika mashindano hayo yaliyofanyikamwisho wa wiki iliyopita katika chuo cha uandishi wa habari cha Royal (RCT), TSJ waliwazidi washindani wake kwa kupata alama za jula 887, wakifuatiwa kwa mbali na RCT waliopata alama 880.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Chuo cha Dar es Salaam City College (DASICO) na DSJ wakiwa ni washindi wa mwisho katika mashindano hayo.

Vipengele vilivyoshindanishwa katika mashindano hayo ya utangazaji ni mwanzo wa habari, kusoma habari, kuandaa vipindi makini, vipindi vya burudani na vya michezo.

Akieleza ushindi huo, Waziri wa Habari serikali ya wanafunzi wa TSJ (TISJOSO), Jestina Joseph, alisema uamuzi wa kuwashindanisha wanafunzi kitaaluma ni mzuri na una lengo la kuwajenga ki elimu zaidi.

“Tunaamini mashindano haya yatakuwa endelevu ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kushindanishwa kujenga uwezo na ubunifu katika taaluma hii ya uandishi wa habari na utangazaji,” alisema Jestina.

Naye Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO, Bwana Hamad Amour alieleza kuwa chuo chao kuliona ni vyema kushiriki katika mashindano haya ili kujenga uelewa wa taaluma hii na kuona jinsi vyuo vingine wanavyofundishwa katika taaluma hii.

Wakati huo huo Amour aliongeza kuwa serikali yake iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza inayotarajiwa kufanyika tarehe 3 September katika viwanja vya Jangwani Sea Breeze na amesema kuwa sherehe hiyo itawakutanisha tena wanachuo wenzao kutoka vyuo vingine hivyo ambavyo navyo vinatoa taaluma ya habari.

“Katika sherehe hiyo ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza kutakuwa na michezo mbali mbali ambayo itawajenga wanafunzi na kuwaandaa wageni walioingia chuoni hapa kwa ajili ya kupata taaluma ya habari,” alieleza Amour.

Aliongeza kuwa mbali na kuburudika kwa michezo mbali mbali katika sherehe hiyo ni wakati wa kukutana pia na waandishi pamoja na wahariri wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa Tanzania kuzungumza nao ili nao watupatie elimu itakayo tuandaaa kuelekea kazini.

“Tunatarajia kualika wadau mbali mbali wa habari ambao tutajumuika nao pamoja katika sherehe hii ili kubadilishana nao mawazo na kujifunza mengi kutoka kwao na pia tutakuwa na mgeni rasmi kutoka serikalini ambaye tutawajulisha badae ni nani atakaye kuja kwani bado tuko katika mawasiliano nae,” aliongeza.

0 comments: