BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Wednesday, September 14, 2011

"KATIBA MPYA INAHITAJIKA KULETA UFANISI WA KAZI" Maembe...

MSANII wa Muziki wa asili nchini Vitalis Maembe amesema katiba mpya inahitajika ili kuleta ufanisi wa kazi hasa kwa wasanii ambao wanahitaji uhuru katika kazi zao.

Maembe alitoa kauli hiyo alipokuwa akitumbuiza katika jukwaa la sanaa linalofanyika kila siku ya Jumatatu, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).


“Tunahitaji katiba inayoendana na mahitaji ya watanzania katika kuleta chachu ya muziki wa asili, katiba isiyo ya kikoloni itakayoruhusu tume huru na itakayotoa uhuru kwa wasanii kutokana na kile wanachokiimba, ” alisema.

Aidha alisema, muziki wa zamani ulikuwa unatumia katiba kwa asilimia kubwa na ndio maana uliweza kufanikiwa ndani na nje ya nchi.

“Maudhui ya kimuziki ni lazima yaendane na katiba kama ilivyokuwa zamani,katiba lazima imfanye msanii kuwa huru na kuimba kile anachokiamini ilimradi asivunje maadili katika kazi yake ya kimuziki”

Alisema kuwa aina ya muziki wake umejikita zaidi katika kutoa elimu dhidi ya rushwa, uvivu kwa vijana kwa kisasa ili kuweza kuleta madiliko chanya katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa wanamuziki ndio kioo katika jamii yoyote ile dunia, na ndio watu wanaoweza kuleta mabadiliko kutokana na kile wanachokiimba kwa jamii husika.

Hivi sasa Maembe anatamba na nyimbo kama Sumu ya teja, Afrika shilingi tano na nyingine nying.

0 comments: