Wa kwanza kulia ni Meneja wa Redds Bi Vick Kimaro akifuatiwa na mmoja wa washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja wakizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.
Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Redds Bi Vick Kimaro akifuatiwa na washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja kutoka chuo cha CBE akifuatiwa na Aloycia Innocent (UDSM) na wa mwisho kulia ni Asha Mohamed (KIU) wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.
Washiriki wa onesho la Redd’s Uni-fashion bash Bi Upendo Kuboja kutoka chuo cha CBE wa kwanza kulia akifuatiwa na Aloycia Innocent (UDSM) na wa mwisho kushoto ni Asha Mohamed (KIU) katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa fainali za shindano hilo kwa wanavyuo wa vyuo vikuu Dar es salaam.
WABUNIFU wa mavazi wapatao 18 na wanamitindo 24 kutoka vyuo mbali mbali jijini Dar es Salaam leo watashiriki katika onyesho la mavazi lijulikanalo kama Redd’s Uni-fashion Bash lilipangwa kufanyika katika ukumbi wa FPA katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Onesho hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original limeghalimu kiasi cha shilingi million 100 katika maandalizi pamoja na zawadi za washiriki kwa nchi nzima.
Tamasha hili litashirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyo katika mikoa minne ambapo Dar Es Salaam ni mkoa wa kwanza ikifuatiwa na Kilimanjaro, Dodoma na Mwanza.
Akizungumza katika uzinduzi wa fainali za onesho hilo kwa Dar es Salaam, meneja wa Kinywaji cha Redd’s Bi Victoria Kimaro alisema kuwa tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo kupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo.
“Wanafunzi hawa wenye vipaji vya ubunifu wamepata fursa ya kuonesha ubunifu wao wa mitindo na hii ni fursa kubwa sana kwao kujitangaza na kudhihirisha uwezo wao,” Bi Kimaro aliongeza.
Bi Kimaro alisema zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hawa ili waweze kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za pesa taslim washindi watano katika kila mkoa watakaoshika nafasi za juu.
Alisema kuwa wabunifu wa mitindo watakao shika nafasi ya kwanza watapatiwa kitita cha Sh 700,000, mshindi wa pili 500,000 na mshindi wa tatu atapaitiwa Sh 300,000 pia mshindi wan ne na wa tano watapatiwa Sh 100,000 kila mmoja.
Aliongeza kuwa wanamitindo watapatiwa Shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza na wa pili atapatiwa Shilingi laki nne akifatiwa na wa tatu ambaye atapatiwa shilingi laki tatu na washindi wa nafasi ya nne na tano watapatiwa laki moja kila mmoja.
“Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia tamasha hili litahusisha burudani mbalimbali za kuvutia kutoka kwa wasanii wa bongo flava ambao ni Roma Mkatoliki na Joh makini na pia hii ni sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali katika kufurahia na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya ubunifu na mitindo,” alisema.
Aliwataja washiriki wa onesho hilo kuwa ni Aloycia Innocent kutoka USSM, Rosemary Osward (CBE), Magreth mhoza (MNMA) Upendo Kuboja (CBE) na Kudra Lupatu kutoka CBE.
Wengine ni Emmanuel Elly kutoka CBE, Lameck Stephen (IFM), Benson Macha (CBE), Saadat Juma (IFM) Conrad Gumbo (IFM), Issack Ibrahim (UDSM), Amos Kalinga (UDSM) na Asha Mohamed kutoka KIU.
Washiriki wengine saba ni Rose Hubert kutoka KIU, Gerald Kalinga (UDSM), Hussein kasim (UDSM), happiness Mushi (CBE), Yalita Malanduzi (UDSM), Brian Abdul (CBE) na Rosa Damazo(IFM)
Bi kimaro pia aliwataja majaji wa tamasha hilo kuwa ni Taji Liundi, Hamisa Hassan, farouk Abdala na Castantine Magavile.
0 comments:
Post a Comment