BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, November 21, 2011

Aslay abadili uchumi wa familia


WAKATI wasanii wengi wa muziki wakiishia kufanya matanuzi kwa fedha za mapato ya kazi zao, kinda wa anayetamba na wimbo wa Nakusemea, Aslay Isihaka, ameamua kubadili maisha ya familia yake kwa kumpa mama yake mtaji mkubwa wa biashara.

Kinda huyo anayechipukia katika muziki wa kizazi kipya, amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukali wa maisha uliokuwa ukiiandama familia yake.

Kuna wakati tulikuwa tunalala na njaa, sasa hatutalala njaa tena, alisema msanii huyo anayesoma Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Tandika.

Nilikuwa naumia sana na kumwonea huruma mama yangu, lakini naimani sasa haya yote yamekwisha.

Aslay ni kati ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Mkubwa na Wanawe, kinachomilikiwa na Saidi Fela, mmiliki wa kikundi cha TMK Wanaume Family.

Kituo hiki kipo maeneo ya Temeke-Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

0 comments: