BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, December 4, 2011

WAKURUGENZI WA TFDA WATUNUKIWA VYETI...

Mshauri wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Legu Mhangwa  akimtunu cheti cha Umiliki katika Uongozi  Adam Fimbo , jijini Dar es salaam. 

Zaidi ya wakurugenzi na meneja 500 kutoka katika taasisi na mashirika zaidi ya 30 nchini wametunukiwa vyeti vya mafunzo ya uongozi kutoka katika taasisi ya Crest Business Trainers.
Kati ya wahitimu hao mwishoni mwa wiki hii meneja na wakurungezi 10 kutoka mamlaka la dawa na chakula (TFDA) walitunukiwa vyeti vya mafunzo ya jaketi la uhimili katika uongozi .
Mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na Crest Business trainers ambao ni wakala wa Crestcom international kutoka nchini marekani yalikuwa ni mafunzo ya siku tano.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya viongozi hao kutunukiwa vyeti,  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Bi Hafsa Mahinya alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kubadilisha mtazamo wa viongozi wa mashirika hasa katika kuboresha utendaji wao wa kazi.
Alisema kuwa mafunzo hayo hutoa elimu katika nyanja mbali mbali katika kuhakikisha utendaji wa kazi wa viongozi hawa unaboreshwa na kuweza kukidhi haja ya mhudumiwa na hata kukidhi haja ya kampuni ama shirika analofanyia kazi.
“Haya ni mahafali ya tisa tangu tumeanza kutoa mafunzo haya na tumeona mafanikio makubwa kwa wahitimu wote waliopata mafunzo haya na asilimia kubwa ya wahitimu wamepanda vyeo kutokana na utendaji wao wa kazi kuboreshwa,” alisema.
Alisema kuwa Meneja wengi hawana muda wa kuwa nao kwa muda wote hivyo wameamua kutenga muda wa saa 48 kwa siku tano ili kuweza kuwapata na kuwapatia mafunzo hayo.
Aliongeza kuwa kati ya mashirika ambayo yaliwahi kunufaika na mafunzo hayo ni pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao walipatiwa mafunzo hayo kwa mara 2 mfurulizo, shirika la mawasiliano ya simu Tanzania (TTCL) ambao wakurugenzi wake wamepatiwa mafunzo yaho mara 4, na kampuni ya simu za mkononi airtel ambayo imepatiwa mafunzo hayo mara 2.
Alisema kuwa mafunzo hayo yenye lengo la  kubadilisha mtazamo wa vingozi hawa ili waende na taratibu za kufanya biashara na aliongeza kuwa mafunzo hayo yalianza kutolewa katika taasisi na mashirika mbali mbali tangu mwaka 2002.
Naye mshauri wa tiba na dawa kutoka TFDA Mr Legu Mhangwa alisema kuwa mafunzo haya yatawawezesha viongozi hawa kuweza kupata matokeo mazuri hasa katika suala zima la kubadilisha mtazamo.
Alisema kuwa ni kazi ya mamlaka kufundisha wafanyakazi ili waweze kutoa huduma bora kwa wanaopokea huduma hizo ambao ni jamii kwa ujumla.

0 comments: