BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, December 17, 2012

Wafanyakazi wa Vodacom watoa msaada kwa kituo cha yatima Friend of Don Bosco Kimara

 wafanyakazi wa mtandao wa simu ya mkononi Vodacom Tanzania kitengo cha Customer care wakitoa msaada wa vitu mbali mbali kama vyakula, vitanda, magodoro vyenye thamani ya Sh6 million.
















Sunday, September 2, 2012

Miss & Mr TSJ 2012 at mbalamwezi beach

 Hao ni washiriki mashindano ya kumtafuta Miss na Mr Tsj kwa mwaka 2012/2013 yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mbalamwezi Beach na hapo wakiwa wanaingia katika steji.
 Wakiwa katika katika steji wakiwa burudisha wanafunzi wenzao kutoka chuo cha uandishi habari kiitwacho Tsj kilichopo Ilala-Sharifu shamba pamoja na Mkuu wao wa chuo cha TSJ akiwa bega kwabega akiongozana na mgeni Rasmi kutoka kitengo cha Haki za kibinaadamu{LHRC}
                                            Washiriki wa MISS na MR TSJ wakiwa katika picha ya pamoja hapo
 Picha ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa pamoja  na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe Bi Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi Frida Matinya.
 Picha ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa pamoja  na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe Bi Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi Frida Matinya.pamoja na Miss na Mr ambao wamewavalisha Taji washindi wa mwaka huu.

Sunday, August 12, 2012

TAMASHA LA DINI "LOVE TANZANIA" LILIVYOTIA FORA VIWANJA VYA JANGWANI JIJI DAR.

Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya chakula uwanja hapo.
Moja ya Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa limepaki katika Viwanja vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa Uwanjani hapo wakati tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiendelea.
Pichani Juu na Chini ni moja ya michezo iliyofanyika kama sehemu ya burudani uwanjani hapo ambapo ilionekana kuvutia Umati wa Watanzania waliohudhuria tamasha hilo.
Vijana, Watoto kwa Wazee wakitazama mchezo wa mapikipiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo kama inavyoonekana.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia mchezo wa Baiskeli.
Palikuwa hapatoshi Jangwani.
Ulinzi na Usalama kwa raia ulikuwepo.
Familia zikiendelea kula, kunywa na kufurahi uwanjani hapo.
Hili ni Jukwaa la kimataifa kutoka nchini Uganda maalum kwa ajili ya Tamasha lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka nchini Marekani, haijawahi kutokea kusikia Sound na Mziki wa Ukweli nchini kwa mliohudhuria tamasha hili mtasema.

Saturday, August 11, 2012

TSJ KUMPATA MRITHI WA MR & MISS TSJ AUGUST 2 PALEEE MBALAMWEZI BEACH




SERIKALI  ya wanafunzi ya chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism (TSJ) inatarajia kuwapata wawakilishi wapya wa taji la Miss na Mr TSJ katika sherehe za ‘Bash’  ambazo zimelenga kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi August tarehe 25 zitafanyika katika uwanja wa Mwalamwezi Beach, na itasindikizwa na wasanii mabli mbali wa muziki wa Bongo flava.
Akizungumza na gazeti hili, Rais wa chuo hicho Bi Frida Matinya alisema kuwa sherehe hizo ni moja ya utaratibu waliojiwekea katika kuwapokea wanafunzi wapya ambao ni wameingia chuoni hapo kuchukua kozi mabli mbali.
Alisema kuwa katika sherehe hizo ambazo zitashereheshwa na michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya mavazi, Mr na Miss TSJ, Kuimba, kuvuta kamba, kuogelea na michezo mingine mingi ya baharini.
“Lengo la sherehe hizo ni kuwa kawaweka karibu wanafunzi wageni na pia kufahamiana pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa wanafunzi wote pia kuwapa burudani pia kujijenga kisaikolojia kwani michezo hujenga, kujumuika pamoja katika hafla hii itatuwezesha kuwa na ushirikiano wa kutosha,” alisema.
MWISHO.

Sunday, June 3, 2012

AMREF Wazindua kampeni haki ya fya ya uzazi kwa vijana



 Keisha aikuzungmza na mmoja wa waelimisha rika ktk viwanja vya  Sinza darajani
 meya wa kndoni yusuph Mwenda na Meshak toka amrefu wakifuatili kwa makini
 wana acrobatic wakifanya vitu vyao uwanjani.
 duh... unamfahamu huyu... nimemkubali sana kwa kazi hii
 jingine hilo
na hii...

Monday, May 28, 2012

Bifu jipya Cyrill, Ommy Dimpoz


BAADA ya msanii aliyevuma na wimbo Nai Nai Faraji Nyembo Ommy Dimpoz kumuua kwa maneno msanii Cyrill, sasa yamemrudi baada ya Cyrill naye kuongea yasiyofaa kumhusu Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz alinukuliwa katika kituo kimoja cha redio akisema kuwa Cyrill ni msanii ambaye hafanyi shoo kabisa.

"Huyu jamaa amekosea kwa kwa kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza tu, siku nyingine ajipange kabla ya kufanya mahojiano yoyote, kwani ukiwa msanii wewe ni kioo cha jamii, haifai kuongea kila linalokuja kichwani mwako" alisema Cyrill

Bifu hili jipya kati ya wasanii hawa limetokana na kuzuiwa kwa Cyrill kufanya show na BASATA siku ya Jumapili iliyopita pale Club Maisha akidaiwa hana kibali kwani ni raia wa Kenya.

Ommy Dimpoz naye alikuwa na shoo yake siku hiyo Billcanas.
Baadaye Ommy Dimpoz alifunguka kwenye vyombo vya habari na kusema Cyrill anatangaza kuwa yeye ndiye kamfanyia fitna ili asifanye shoo hiyo, jambo alilokanusha.

Serikali yataka maombi ya uchunguzi wa umri wa Lulu yatupwe

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba umepinga maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu kuhusu umri wa mshtakiwa huyo na kuiomba mahakama hiyo iyatupilie mbali.

Pingamizi hilo la awali liliwasilishwa mahakamani hapo jana na mawakili wa upande wa mashtaka Elizabeth Kaganda na Shadrack Kimaro mbele ya Jaji Dk Fauz Twaib wakati wa kusikilizwa maombi hayo.
Akiwasilisha pingamizi hilo, wakili Kimaro alidai kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kinyume cha sheria.

Alidai kuwa hata vifungu vya sheria namba 120 (ii) na 113 (i) na (ii) vya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambavyo upande wa utetezi umevitumia kuwasilisha maombi hayo haviipi mamlaka mahakama hiyo kuweza kusikiliza maombi hayo.

“Namna walivyowasilisha maombi yao na sababu walizozitaja hazitoshi kuiruhusu mahakama hii kusikiliza maombi yao,”alidai Kimaro na kuongeza kuwa:

“Ni kweli kwamba mahakama hii ina uwezo wa kusikiliza suala la umri, lakini namna upande wa utetezi walivyowasilisha maombi yao hakuiwezeshi mahakama hii kuyasikiliza,”alidai.

Kimaro alidai kuwa mojawapo ya kielelezo kilichowasilishwa na upande wa utetezi wakidai ni uamuzi uliotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu si uamuzi bali ni amri ya mahakama.
Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi Kenedy Fungamtama ambaye alikuwa akisadiana na Fulgence Massawe na Peter Kibatala, alidai kuwa maombi yao ni ya msingi kwani wamefuata taratibu zote za kisheria na kuomba mahakama iyasikilize.

“Tulichofanya tumefanya kwa kufuata amri iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kilichoko hapa ni ubishi kuhusiana na umri wa mshtakiwa,”alidai Fungamtama na kuongeza kuwa:

“Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikutoa uamuzi bali ilitoa amri kwa mawakili wa mshtakiwa kama wana maombi yoyote wafanye hivyo kupitia mahakama kuu na ndivyo tulivyofanya,”alidai.

Wakili huyo wa utetezi aliendelea kudai kuwa, hata katika sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imetafsiri neno mahakama ikimaanisha kuwa ni ile ya mwanzo, wilaya, mkoa ama mahakama kuu hivyo ni sahihi maombi yao kuwapo mahakamani hapo.

“Upande wa mashtaka wameshindwa kuisaidia mahakama hii ni taratibu zipi ambazo hatukuzifuata katika kuwasilisha maombi haya hivyo pingamizi lao litupiliwe mbali,”alidai Fungamtama.

Upande wa utetezi pia ulinukuu kesi mbalimbali zikiwamo rufaa ya madai namba 86/2009 kati ya Samson Mwalida na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na  kati ya Farida na Kampuni ya Scania Tanzania Ltd.

Jaji Twaibu baada ya kusikiliza hoja zote, aliwauliza maswali.Jaji: Je mnadhani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi haya?
Jaji: Nikiangalia kumbukumbu katika jalada hili wakili Kaganda (upande wa mashtaka) alisema Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza maombi haya kwasababu kesi iliyoko mbele yake ni ya mauaji ambayo husikilizwa na mahakama kuu.

Kaganda: Mtukufu Jaji mimi nilisema hivyo nikimaanisha kwamba bado tunaendelea na upelelezi na kati ya vitu tunavyochunguza ni pamoja na suala la umri wa mshtakiwa.
Baada ya kusikiliza hoja zote Jaji Twaib aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 11 mwaka huu atakapotoa uamuzi kuhusiana na maombi hayo.

Upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ukiiomba mahakama kuu iangalie na kuona kama mahakama ya kisutu ina uwezo wa kuamua suala hilo.

Sunday, May 27, 2012

MWAKYEMBE AVAMIA TAZARA SAA 4 USIKU, Ni baada ya kupata taarifa kuwa treni ya mchana haijaondoka. Asema Uzembe wa watendaji ndio unasumbua abiria. Akaa Tazara mpaka Treni ilipoondoka Saa 6:00 usiku.


 Kiza cha wastani kimetanda kabla Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe hajawasili TAZARA.
 Mara Daktari anawasili kutaka kujua kunani?
 Akipewa maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kanda Abdalla Shekimweli baada ya kutaka maelezo kwanini Treni haijaondoka hadi saa nne badala ya saa nane mchana.
 Akiwasikiliza kwa makini viongozi hao waliokua wakihaha kutoa majibu yakueleweka.
 Shekimweli akijitahidi kunyoosha maneno ili waziri amuelewe.
 Hapa waziri akaona bora waende wakalione hilo treni lenyewe!
 Dk. Mwakyembe akizungumza na abiria wa usafiri huo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa vingozi, nakuwaambia hakuna sababu yoyote ya maana iliyofanya wasiondoke ila ni uzembe tu. Amegundua kuna uwozo mkubwa kwenye menejimenti ya Shirika hilo ndio maana matatizo ya mara kwa mara yanatokea, huku abiria hao wakimshangilia. Mimi sikuwepo hapa nchini nimerudi jioni hii kutoka India lakini kuna abiria kama wawili wamenipigia kunieleza taarifa hizi ndiyo maana nimekuja kujua tatizo nini na nimegundua ni uzembe tu. Sababu kubwa iliyoelezwa ni kutokuwepo kwa mafuta lakini ni uzembe tu nitaushughulikia hivi karibuni.
" Kama shirika hili lingekua mali ya watanzania tu pekeyao basi sasa hivi ningetoa maamuzi usiku huu na nyie mngeona, lakini hatua ninayo ichuku sasa nimewaambia nataka treni iyondoke haraka mwisho iwe saa sita kuwepo abiria hapa! na siondoki hadi na hakikisha treni inaondoka," alisema Dk. mbele ya wananchi hao pichani.


 Abiria wa VIP nao alizungumza nao.

 Abiria wakichungulia kwa mbali wakati Dk. Mwakyembe alivyo akiwasulubu kwa maswali viongozi wa Shirika hilo.
 Mara abiria wakaanza kuitwa kupanda treni.
 Raia wa kigeni nao walikuwepo wakisota tangu saa nane mchana hadi mida hiyo ya saa sita usiku, huku Dk. Mwakyembe akiwaaga na wao kumpongeza.
 Tunakushukuru waziri bila wewe hapa tunge lala hapa! walisikika wakisema baadhi ya abiria.
 Baada ya abiria wote kuingia akapita kila behewa kuangalia kinachoendelea, hadi inaondoka.
 Hapa Dk. Mwakyembe anasubiri kichwa cha treni kije kuunganishwa ili liondoke. Baada ya kupata maelezo kuwa kinawekwa mafuta maeneo ya Yombo.
 Hapa zikionekana taa za kichwa hicho zikiwasili kwa mbaaali.
 Na sasa kimewasili rasmi kichwa.
 Kinaunganishwa taratiibu na treni.

Hatimae safari ikaanza na furaha ikitawala.