Amina Sangawe
Anitha Kitobero (Miss TSJ 2011)
Rose Pilliad
Christina Dodo
Winnie Urio
Tumaini Mapasa
Alice Donatus
baadhi ya washiriki wa Miss TSJ katika pozi baada ya kumaliza mazoezi ya maandalizi ya shindano hilo.
Wakati mashindano ya Miss Tanzania yanatarajiwa kuanza hivi karibuni katika hatua za awali, mapema mwezi huu chuo cha uandishi wa habari cha Time School of journalism (TSJ) kinatarajia kumpata mrembo atakaye tununikiwa taji la Miss TSJ 2012.
Mshindi wa kinyang’anyiro hicho anatarajiwa kupatikana tarehe 10 March katika hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Belinda Beach maeneo ya Kawe wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari, makamu wa Rais wa uongozi wa wanafunzi wa chuo hicho Bi Zainab Mlawa alisema kuwa tayari wamekwisha pata warembo ambao wameanza maandalizi kwa ajili ya kuelekea katika fainali hizo.
“Tayari tuna warembo 11 ambao watachuana katika sherehe hiyo na mpaka hivi sasa maandalizi ya mashindano ya Miss TSJ pamoja na sherehe hiyo yapo katika hatua za mwisho,” alisema.
Bi Mlawa alisema kuwa katika kumtafuta mshindi wa taji hilo tayari uongozi wa serikali ya wanafunzi (TISJOSO) imekwisha panga jopo la majaji ambao ni wadau wa muda mrefu katika tasnia hii na wanatarajia kuwatangaza majaji hao pamoja na zawadi za washindi hivi karibuni.
Alisema kuwa sherehe hiyo imeandaliwa na serikali ya wanafunzi ya Time School of Journalism (TISJOSO) na itajulikana kama Welcome First Year Special Bash ambayo imelenga kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya cheti, stashahada kwa mwaka huu.
Bi Mlawa alisema mashindano ya mwaka huu ni mashindano rasmi na yako tofauti na mashindano yaliyowahi kufanyika hapo awali. Kwa kuwa mashindano yaliyokuwa yakifanyika mwanzoni yalikuwa hayana tija kwa washiriki kwani hayakuwawezesha kupiga hatua yoyote ya kuendeleza kipaji hicho licha ya kuwa kuna baadhi ya waliofanikiwa kuendelea katika tasnia hiyo.
“Mpaka hivi sasa washiriki waliojitokeza ni 11 na tunazidi kuwahimiza wajitokeze kuchukua fomu ili washiriki katika mashindano hayo na wao watambue kuwa mashindano haya humpatia cheti cha heshima mshindi, na mbali na zawadi pia cheti hicho ni kama utambulisho ambacho kitampa nafasi ya kuonyesha ushiriki wake katika mashindano hayo,” alisema.
0 comments:
Post a Comment