Mshindi wa nne katika shindano la Anzisha Price 2011, Fredrick Swai (Kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa vyuo mbalimbali walihudhuria mkutano wa kujadili mradi wa Anzisha Prize wakishilikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania kuendesha shindano la kutafuta vijana wenye ubunifu hasa katika kuleta mapinduzi ya teknolojia
TUME ya Sayansi na Tekinolojia Tanzania (Costech) kwa kushirikiano na African Leadreship Acadeemy (ALA) ya Afrika ya Kusini wameamua kuinua vijana wa hapa nchini kwa walio na ubunifu wa kisayansi ili kuweza kujenga uwezo vijana kumudu na kuzitatua changamoto mbalimbali za kijamii.
Kupitia tuzo za Anzisha prize ambazo zilianzishwa mwaka jana na kuhusisha nchi zaidi ya 23 barani Africa itawawezesha vijana kutoa mawazo yao kwa kufanya vitu mbalimbali vitakavyo weza kutatua matatizo katika jamii.
Akizungumza na wandishi wa habari jana Mkurugezi wa habari na nyaraka kutoka COSTECH Raphael Mmasi alisema kuwa vijana wengi wa kitanzania wana ndoto japokuwa hawana pakuwezesha ndoto hizo, na kutokana na pato la nchi kuwa dogo na kutofikia malengo inachangia vijana wengi kujiingiza kwenye mambo yanayosababisha wengi kupoteza ndoto zao
“Tumeanzisha mpango huu kwa makusudi ya vijana wa Afrika nzima kutimiza ndoto zao zisipotee bure na moja ya majukumu yetu ni kuibua vipaji vya Sayansi”alisema Mmasi.
Alisema kuwa mradi huo utahusisha vijana wenye umri wa miaka15 mpaka20 ambao wameweza kubuni kitu chochote kinachoweza kutatatua changamoto zinazoikumba jamii inayomzunguka.
Alisema kuwa mwaka jana walifanya shindano hilo na Joel Mwale kutoka Kenya alikuwa mshindi wa kwanza, mwaka huu mshindi wa kwanza atapatiwa dola elfu75 kama zawadi na mashindano yatafanyika hivi karibuni nchini Afrika ya kusini.
Bw Mmasi alisema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanategemea umeme unaozalishwa na maji, hivyo kupitia mawazo mbalimbali yatakayotolewa na vijana hawa yataweza kutatua kero hiyo na kupendekeza njia mbadala za kuzalisha umeme mfano kupitia jua na rasilimali zingine.
Fredirick swai(20) ambaye ni mshiriki wa shindano hilo la mwaka2011 kutoka Tanzania alisema kuwa kwa mwaka huu wanatarajia kupata maombi mengi zaidi kuliko mwaka jana maombi yalikuwa 180 kutoka nchi 23 za Afrika.
Katika walsha iliyo fanyika jana walipokea wanafunzi 70 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kwa siku ya leo wanatarajia kutembelea shule ya sekondari oyersterbay kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa tuzo hizo.
0 comments:
Post a Comment