BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Friday, July 23, 2010

Foxy Brown chini ya ulinzi baada kukwaruzana na Jirani yake


Rapper Foxy Brown amefunguliwa mashtaka baada ya kukwaruzana na jirani yake hivi karibuni, kwa mujibu wa NY Daily news rapa huyo alizinguana na mwanamke ambaye tayari alikua na kinga ya mahakama dhidi ya Foxy Brown, kitaalamu inaitwa order of protection, kutokana na tukio lililotokea mwaka 2007 ambapo Foxy alituhumiwa kwa Kumpiga mwanamama huyo na Simu ya Black Berry Inasemekana na wawili hao walipishana, yaani Foxy na Arlene Raymond, sasa basi Arlene alimwangalia Foxy, ndipo Foxy akamind na kumfokea What the **** are you looking at?" ukiipunguza makali inakua kama “we bwege unamwangalia nani?”

Baada ya kuambiwa hivyo jirani sijui aliogopa moyoni au ndo akaamua kumkomesha hasimu wake? Basi akapigia simu polisi, na wakaja kumkamata Foxy Brown, na kesi imeanza upyaaa. Foxy Brown hakuweza kupatikana ili acomment juu ya ishu hiyo.

0 comments: