Tashera Simmons ametangaza kutengana na Rapa Earl Simmons a.k.a Dmx, na wakati huo huo anajiandaa kushoot kipindi cha Television/Reality show kinachohusu maisha halisi aliyopitia ndani ya ndoa yake na rapa Dmx hasa jinsi familia hiyo ilivyopigana na maisha wakati rapa huyo alipokuwa amebobea na madawa ya kulevya, pamoja na uhalifu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Tashera amesema katika Kipindi hicho pia ataelezea jinsi gani DMX alivyokuwa haijali familia yake. Mwanamama huyo anasema alianza mahusiano na Dmx Kuanzia akiwa na umri wa miaka 11 na alipofikisha miaka 18 ndipo alipoanza kuishi nae mpaka hivi karibuni alipotoka jela.
Tashera ameanzisha foundation inayoitwa WOMEN OF STRENGTH ambayo ni maalum kwa ajili ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, na unyanyasaji anaoupata mwanamke nyumbani. BADO Dmx hajajitokeza kuzungumzia ndoa yake, lakini mara ya mwisho alionekana wiki iliyopita, alipoungana na Kina Lil Kim katika kuperform ngoma ya kitambo sana inayoitwa Money Power Respect, jijini Newyork
0 comments:
Post a Comment