BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, July 10, 2010

MKALI WA CINDELELLA ALIKIBA

Staa wa ngoma ya Cinderela aliyejiajiri kupitia game ya muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva, Ali Kiba anachana wazi kwamba dhuluma inayofaywa na baadhi ya mapromota wa kibongo ndiyo sababu kubwa inayomfanya kuzipa kisogo ‘shoo’ za Kibongo na ‘kulowea’kwenye steji za Ughaibuni.

ALI K

Mkali huyo ambaye bado anauza kupitia kazi zake za muziki hapa ‘Tizii’ na nchi za jirani, amedai kuwa alikumbwa na matukio mengi ya kudhulumiwa mkwanja wa shoo na mapromota uchwara wa Kibongo, kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza, akaamua kuziweka kando kwa muda shoo za kibongo

“Kuna watu fulani fulani hivi wanawaumiza sana wasanii, huku wakitangaza kuwasaidia na kuwainua, lakini ukweli ni kuwa jamaa ni watu wa dhuluma sana ndiyo maana mimi nakamua mbele kwa mbele ambako hakuna longolongo,” alitanabaisha staa huyo aliyewahi kukimbiza na ngoma yake, ‘Usiniseme.’

0 comments: