BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, July 10, 2010

SARAH KAISI NA MUZIKI!.

Staa wa ngoma ya Shoga, Sara Kaisi a.k.a Shaa amefunguka na kuweka wazi kwamba, hivi sasa anaweza kuisaidia familia yake wakiwemo wazazi kwakuwa tayari ameshaanza kuchungulia mafanikio kupitia game ya muziki wa kizazi kipya.

SHAA

Akihojiwa na kituo kimoja cha Radio...hivi juzi kati,Shaa alisema sanaa ya muziki ambayo aliianza tangu 2004 hivi sasa imemfanya aishi vizuri huku akiisaidia familia yake kwa mambo mbalimbali ikiwemo kuleta misosi mezani.

“Huko nyuma wakati naanza muziki sikuwa na uwezo wowote, lakini sasa naweza kuwasaidia hata wazazi wangu,” alisema Shaa ambaye hivi sasa anafanya vizuri na kupitia kazi hiyo.

0 comments: