BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, July 18, 2010

Mwisho Ndani ya Nyumba!!!

Shindano la Big Brother Africa 5 limeanza huko Mwisho Mwampamba akiwakilisha Tanzania ndani ya jumba la Big Brother. Mwisho aliwahi kushiriki katika shindano la kwanza kabisa la Big Brother mwaka 2003 na alijipatia umaarufu mkubwa alipoibuka mshindi wa pili nyuma ya kimwana Mzambia Cherise Makubale, aliyeibuka mshindi na kuzoa zawadi ya dola 100,000 (sawa na Sh. Milioni 130).



Baada ya Watanzania kuikosa kwa hatua chache tuzo hiyo ya BBA1, mashindano hayo ya runinga yalisimama kwa miaka minne na yaliyoporejea 2007, Richard Bezuidenhout, akafanya mambo. Akawa mshindi wa Big Brother Africa 2, akiwaacha washindani wake Tatiana, ambaye alikuwa mpenzi wake wa ndani ya jumba la BBA na Mnigeria Ofunneka, wakishika nafasi ya pili na ya tatu.
Mwaka uliofuata, Tanzania iliwakilishwa na Latoya Lyakurwa (2008) na Elizabeth Gupta (2009) ambao walitolewa mapema.
Wadau mnaonaje, Mwisho ataweza kujishindia hizo dola laki 2??

0 comments: