Baada kimya cha muda sasa,mwanadada Baby Madaha,ambaye pia ni chimbuko la Bongo Star Search (BSS) hivi karibuni amerelease single mpya aliyoipa jina DESPERADO...kazi ikiwa chini ya Producer Allan Mapigo.
Kwa mujibu ya mrembo huyu,single hiyo itakuwa moja ya track zilizomo ndani ya sound track ya kampuni la PILIPILI INTERTAINMENT ambayo itaitwa OBSESSION.
Alipoulizwa wimbo Desparado unazungumzia nini haswa,mwadada huyu alisema....
"Kwanza watu wataipenda kwasababu nimeimba kuhusu upande wa pili wa Mapenzi, unampenda mtu na unampa yote halafu tena hakujali, matokeo yake napata mwingine halafu yeye anarudi tena, hapo ndo ndipo ishu inapokuwa nzito." alimalizia fashionista huyo.
0 comments:
Post a Comment