Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Galawa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ‘Usiku wa Kanga za Kale’ utakaofanyika Oktoba mosi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, tamasha hilo litashirikisha wabunifu wa mavazi na wadau mbalimbali, wakiwemo kina mama na kina baba watakaopanda jukwaani kuonyesha mavazi ya kanga na vionjo.
Idarous alisema tamasha hilo litasindikizwa na burudani kutoka kundi la Jahazi Modern Taarab, waimbaji nyota Khadija Kopa, Rukia Ramadhani, Sabah Salum Muchacho na Baby Madaha.
Aidha, Idarous alitaja viingilio katika usiku huo kuwa ni shilingi 20,000 kwa viti maalumu ‘VIP’ na shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida, ambako tiketi zinapatikana Fabak Fashions.
usiku huo wa kanga wataoonesha mavazi ni macelebrity wa bongo wakiwemo waigizaji wa filamu, wadau wa mitindo na watu kadhaa wanaofahamikatika sekta tofauti tofauti
0 comments:
Post a Comment