BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, December 13, 2010

DK REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA.


Habari za kusikitisha zilizofikia leo asubuhi hii ni kwamba msanii maarufu hapa Tanzania mwenye asili ya kiZaire, Dr. Remmy Ongala, amefariki dunia.
Inasadikika kwamba Ongala alipelekwa hospitali kuu ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kuzidiwa usiku wa Jumapili. Alitangazwa marehemu mapema Jumatatu baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya na madaktari kushindwa kumsaidia.
Remmy Ongala atakumbukwa zaidi kwa ustadi wake kwa kupiga guitar na uimbaji wake ambao uliweza kuzivuta hisia za wengi kwa miaka 30 aliyokuwa akishughulika na muziki.
Tunaiombea familia ya Dr. Ongala faraja na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

0 comments: