BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, December 13, 2010

FAINALI YA BSS 2010 KUFANYIKA IJUMAA.


HATIMAYE washiriki watano wameingia fainali za shindano la Bongo star search na watachuana kumtafuta mshindi katika fainali itakayofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam.
Washiriki hao wameingia katika hatua hiyo baada ya washiriki wenzao watatu kutangazwa kuaga shindano hilo jana wakati walipofanya 'shoo' kwenye ukumbi wa Water front na kurushwa na kitua cha televisheni cha ITV.
Shoo hiyo ilipambwa na wasanii nyota kadhaa wakiwemo Banana Zoro, Mwasiti, Tundaman, Maunda zoro, Amini, Barnaba, Marlaw na Patricia hilal, amabo waliimba pamoja na washiriki wa BSS.

Washiriki watano walioingia katika fainali hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi kutoka kwa wananchi ni Waziri salum, Bella Kombo, James Martin, Joseph Payne na Mariam Mohamed.
Washiriki watatu walioaga michuano baada ya kupata kura chache ni Christabella nzowa, Haji Ramadhani na Chiby Dayo.
Mshindi wa BSS mwaka huu atajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 30.

0 comments: