BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Wednesday, September 7, 2011

UAMINIFU WAKE WAMPUNGUZIA SKENDO.. Jonwoka

“UAMINIFU katika mahusiano ndio unaonifanya nisiwe na orodha ya skendo katika maisha yangu, ukizingatia kazi zangu zinanikutanisha na majaribu mengi,”.


Ni kauli ya msanii gwiji wa muziki nchini Michael Denis a.k.a Joni Woka, ambaye alitamba sana awali akiwa na Wagosi wa Kaya katika albamu ya Ridandasi za Majungu.


Woka anasema, tangu alivyoanza kazi yake ya muziki na kuwa na mahusiano ya kimapenzi hajawahi kuwa na skendo yoyote na kwamba amekuwa mwaminifu na kuweza kuheshimu hisia zake.

“Tangu nianze muziki uhusiano wangu wa kimapenzi umekuwa na uaminifu na ndio sababu sijawahi kuwa na skendo hata moja, namshukuru Mungu kwa kuwa hivi sasa natarajia kuingia kwenye ndoa na kuachana na masuala ya girl friend,” anasema.

Anasema, kutokana na maisha ya wasanii wengi kuwa ya kwenda kwenye kumbi za starehe hatakama hawana kazi muhimu na ndio sababu ya kuwa na skendo nyingi ambazo zinaharibu uhalisia wa mtu mwenyewe.

0 comments: