BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Sunday, September 4, 2011

Msanii Sagna kamkimbia mganga


MSANII chipukizi kutoka studio ya Tetemesha Recordz ya jijini Mwanza, Sagna Mganga ametoa wimbo mpya aliouita 'Yamenishinda' ambao ni mwendelezo wa wimbo wake unaotamba wa 'Mganga'.

Akizungumza na gazeti hili meneja wa msanii huyo, Kidy Bwoy alisema wimbo huo mpya ni mwendelezo wa wimbo wa mganga ambao anaeleza jinsi alivyopanga kwenda kwa mganga kwa ajili ya mpenzi wake lakini kutokana na masharti ya mganga ameshindwa kutimiza.

Katika wimbo huo Sagna anashangaa kwa nini mganga amwambie kuwa anadawa ya mapenzi ya kumtibu wakati mganga mwenyewe ameachwa na mkewe na yeye ni mganga, ameshindwaje kuzuia asiachwe.

Kutokana na kushangazwa na masharti ya mganga ndiyo kunampa mwanya wa kufikiria kwa upana zaidi hadi anatambua kuwa mganga huyo ni muongo au dawa zake zimeisha makali kwa kuwa kuna vitu ameshindwa kujitibia mwenyewe ikiwemo kuachwa na mkewe wakati anatangaza kuwa anadawa ya mapenzi.

Licha ya kutoa wimbo huo ameahidi kuwa anakamilisha vide za nyimbo zake mbili za 'Mganga' na huo wa 'Yamenishinda'.

0 comments: