ULIKUWA usiku na hamasa kubwa kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam wakati Maryvine Peter kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM)na Benson Macha kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Jumamosi iliyopita kuibuka washindi katika katika shindano la Redds uni-fashion bash liliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ukumbi wa FPA.
Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Bi Maryvine ambaye alipatiwa kitita cha shilingi laki tano na kufuatiwa na Bw Macha ambaye alipatiwa shilingi laki tatu ambapo Asha Mohamed kutoka chuo kikuu cha Kampala international University (KIU) kushika nafasi ya tatu nao Yusuph Fanuel na Aloycia Innocent walishika nafasi ya nne na ya tano.
Mbali na wanamitindo hao kushika nafasi za juu katika shindano hilo pia mbunifu Esther Amos kutoka CBE alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika wabunifu wa mavazi akifuatiwa na Jackson Gumbala toka (UDSM) ambaye alikuwa katika nafasi ya pili.
Watatu wengine pia walipata nafasi ya kuingia katika rekodi kwa kuchukua nafasi mbalimbali kama Reznalda Msaki ambaye alikuwa katika nafasi ya tatu na kufuatiwa na Miriam kutoka IFM na Shaaban ambaye alikuwa wa tano.
ushindi lilipatikana katika kundi kubwa la washiriki ambao walikuwa wabunifu18 na wanamitindo 24 kutoka vyuo vikuu mbalimbali na taasisi za elimu ya juu.
Kwa mujibu wa waandaaji wameeleza kuwa kiasi cha Shilingi milioni 100 zimetumika katika uhamasishaji nchi nzima na utoaji wa zawadi kwa washindi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili wakati wa tukio hilo, Meneja wa Redds Bi Victoria Kimaro alisema tukio hilo lina lengo kuu la kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa chuo ambao wameonyesha shauku katika sekta hiyo.
"Tunatarajia kufanya tamasha kama hili Kilimanjaro siku ya Jumamosi ijayo na maandalizi yote ya tukio yamekamilika na baada ya kumaliza Kilimanjaro tutaelekea Mwanza na Dodoma katika wiki zijazo," alisema.
Alisema kuwa washindi katika nafasi za wabunifu walipatiwa Sh 700,000 na mshindi wa pili alipatiwa Sh 500,000 na mshindi wa tatu alipatiwa sh 300,000 huku wale ambao wameshika nafasi ya nne na tano walipatiwa Sh 100,000 kama kufuta jasho.
0 comments:
Post a Comment